Ni kitu gani kimesababisha Dar na Mbeya kushika mkia kidato cha nne?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,216
3,692
Kwanza kabla ya yote ningependa kutoa pongezi kwa wana Njombe na Iringa kwa kufanya vizuri na kuongoza.

Sasa siku ya leo ningependa tujadili ni kuhusu mkoa wa Dar ambao umefanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne na mkoa Mbeya ni kitu kilichosabibisha.

Hii ni mikoa ambayo inaaminika kuwa na wasomi wengi, vyuo vikuu vingi lakini pia upatikanaji wa material upo kwa wingi .

Hivi kuna tatizo gani hapa Dar lakini pia na Mbeya kufanya vibaya.
 
Hivi hizo shule zilizoshika mkia niza serikali au Binafsi? Kwanza tuanzie hapo.
 
zipo hadii privateee mbonaa
Private hatuna shida nazo maana kikubwa wanaajiri wanafunzi waliomaliza form six kama walimu na mishahara ni midogo sana, na hata mazingira ya shule nyingi ni mabovu bora hata za serikali. Lawama ni kwa wizara husika kushindwa kusimamia. Je tatizo kwenye shule za serikali nini?
 
Lawama zote zimuendee JPM kwa kusitisha ajira za walimu, shule zilizofanya vibaya zote ni za serikali waliwekeza nguvu kubwa kwenye madawati na kudhibiti utoro lakini hawakuwekeza nguvu kwenye jira za walimu, sasa shule ziliongoza kwa mahudhurio lakini pia waliweka kukaa kwenye madawati ila walimu wa kuwafundisha hawapo sasa wanafuzi watalaumiwaje wao wenyewe? kama watoto wanapenda singeli mbona FEZA nayo ipo Dar lakini wamefaulu? Ajira kwa walimu ni jambo muhimu kuliko madawati.
 
Tatizo in wanafuzi hawasomi na pia inatokana na uwepo Wa wanafunzi wengi hivyo walimu Wanashindwa kuwamudu
 
Tatizo in wanafuzi hawasomi na pia inatokana na uwepo Wa wanafunzi wengi hivyo walimu Wanashindwa kuwamudu
 
Kwanza kabla ya yote ningependa kutoa pongezi kwa wana Njombe na Iringa kwa kufanya vizuri na kuongoza.

Sasa siku ya leo ningependa tujadili ni kuhusu mkoa wa Dar ambao umefanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne na mkoa Mbeya ni kitu kilichosabibisha.

Hii ni mikoa ambayo inaaminika kuwa na wasomi wengi, vyuo vikuu vingi lakini pia upatikanaji wa material upo kwa wingi .

Hivi kuna tatizo gani hapa Dar lakini pia na Mbeya kufanya vibaya.
VISINGELI VINAHARIBU SANA WATOTO NA JAMII KWA UJUMLA..
 
wanafunzi na baadhi ya walimu wanawaza kubeti na kukaa mitandaoni mda wote ... ila wazazi tuachane na usasa tuwe wakali mitoto isome na kujifunza maisha.. sasa mtoto amefeli shule maisha nayo hakuna dalili za kufaulu kwa kweli tuna kazi
 
Madogo sikuhizi hawatii mixuli , maana nikikumbuka kitambo hichoo mixuli yang, mchikichini kwa sana alafu kutwa nzima nashindia kashata na maji ya kandoro na pesa ya tution na jibana mwenyewe kwenye nauli siombi kwa mzazi. Sikuhizi madogo Mapenzi
 
Back
Top Bottom