Ni kitu gani kilishakuaibisha katika maisha hutakisahau

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,874
3,306
Ilikuwa Jana mida ya saa kumi jioni nilivyotoka kazini nikakuta nyumbani kunawageni shemeji zangu wawili na mama mkwe pia alikuwepo mzee Abdallah jirani angu.

Basi bwana,nikafika nikawasalimu vizuri tukazungumza mawili matatu badae chakula kikawa tayari tukajumuika mezani tukapata chakula vizuri tu.

Tulipomaliza kula tukaendelea na story hapo sebuleni tena zilikuwa zimekolea kwelikweli baadae sauti ikitokea chumbani ikiita mama mama mama! Nikamuona mwanangu mdogo akija sebuleni tulipokaa, mama mimi avaa chupi ako njuri.

Ukweli nilishikwa na aibu kwelikweli ili kuua soo mimi nikamwambia peleka nguo ya dada yako ndani mwanangu,yaani story zilikata kila mmoja akawa kakata mood nikamuona mzee Abdallah ameaga.

Sijui hiyo nguo mtoto aliitolea wapi tangu Jana nikifika nyumbani nakoswa amani kwa kile alichokifanya mtoto mbele ya mama mkwe na shemeji zangu.
Nahisi hii sitaisahau kamwe, je wewe ndugu ni aibu gani nawe hutaisahau.

Karibuni.
 
Hiyo chupi kwani ilikuwa ya rangi gani kama unaweza kuweka picha yake itakuwa vizuri zaidi maana usituletee story za kusadikika
 
Yaani hii ishu unaona aibu? Chupi kaiona muuza duka ije kuwa mama na baba mkwe na mzee Abdallah wakati wao wenyewe chupi zao zimechoka.
Teh teh braza ivi kweli mbele ya mama mkwe? Hii imetokea kweli not jokes
 
Watu kujua kwingi, kutapotosha umaarufu wa Jf humu. Na ndio maana sishangai wale waandishi na wachangiaji nguli humu, hawajitokezi sana siku hizi.

Yaani mwenzetu katoa maada yake, kauliza kama nawe una yako aibu, itoe ili wengine tucheke, tujifunze, pia kufurahisha genge, badala yake mnamponda na kumsanifu.

Ki-ukweli sio poa hata kidogo. Tubadilike, kama huna hoja, soma na upite kimya kimya. Ndiyo Ustaarabu huo.

Ahsante!
 
Hahahahaaaaa!! Kuna day nilipaisha ndege ya kivita(konyagi) bapa1 na mtoto wake, Captein Ndege ikanishinda nikavamia muke ya mutu bar!! Aisee konyagi ctaki kuisikia
 
hodiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mimi yaliyoniaibisha ni mengi, ila jambo moja ninalolikumbuka ni;

Katika mwaka wa balehe yangu, nilimuandikia binti barua ya kimapenzi, nikampa mdogo wake wa kike ampelekee dada yake.

Sasa unajua yule mdogo wake sijui ilitokea nini aisee, wakati anamkabidhi dada yake barua ile (kipindi hicho ni barua, sio msj siju whatsapp, nk kama sasa), mama yao akaona ule mchezo, akaitaka ile barua na akaisoma.

Akamchukua yule mwanae mlengwa na ile barua, akaja nae nyumbani mbio mbio, maana tulikuwa jirani.

Akawakuta wazazi walikwisha rudi, Baba akakasirika sana na alinipandisha juu ya meza, nilichezea fimbo za nguvu aisee, mbele ya yule binti na mama yake. Aiseee nililia sana kwa mengi, ikiwemo aibu.

Ahsante!
 
Kama Kuna watu nimeboa pengine kuwakwaza mnisamehe nami ni binadamu ninamapungufu yangu naona baadhi mnatokwa na povu utafikiri umelazimishwa ukoment kwenye huu Uzi...pita kimya kimya kama hapakufai
 
Watu kujua kwingi, kutapotosha umaarufu wa Jf humu. Na ndio maana sishangai wale waandishi na wachangiaji nguli humu, hawajitokezi sana siku hizi.

Yaani mwenzetu katoa maada yake, kauliza kama nawe una yako aibu, itoe ili wengine tucheke, tujifunze, pia kufurahisha genge, badala yake mnamponda na kumsanifu.

Ki-ukweli sio poa hata kidogo. Tubadilike, kama huna hoja, soma na upite kimya kimya. Ndiyo Ustaarabu huo.

Ahsante!
Nashukuru mkuu ukweli wote umeusema hii si lazma uchangie kama maada hujaependa...wanaboa kwel...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom