Kama alivyosema
ymollel ni kuwa Simu yako imeongiwa virusi. Kirusi au computer Virus ni aina ya program zilizoandikwa kwa nia ovu - kufanya computer, simu au kifaa chako chenye au kinachotumia computer kisifanye kazi tarajiwa na Kukupa majibu yasiyotarajiwa au kuharibu kabisa kifaa chako!
Program hizi Za virusi huandikwa Kila siku lakini uzuri Pia ni kuwa kuna Watu na makampuni makubwa huandika program zinazoweza kung'amua hivyo virusi na kuvitoa kabisa. Program Hizo huitwa Antivirus. Hizi antivirus Pia zinatakiwa Kila Mara kupokea viimarisho (updates) hasa Kutoka ktk mtandao wa internet kwa ajili ya kutambua aina ya virusi vipya vinavyotumwa ktk mtandao wa internet Kila siku!
Kwa hiyo tafuta computer ambayo ina Antivirus ambayo ni hai (updated), Tumia USB Cable iliyokuja na Simu yako, chomeka ktk Simu na kisha chomeka Kwenye computer. Kwenye Simu yako ruhusu computer iitumie Simu yako kama "storage media". Tumia antivirus ya computer kuscan (na kutoa) virusi.
Ikimaliza kabla chomoa Simu yako lakini kabla hujafanya kitu nenda play store na tafuta antivirus yoyote (mfano avg antivirus) uinstall ktk Simu yako.
Fanya hivyo itakuwa imekusaidia kuondoa Hilo tatizo.