Ni kipi wakionacho wao Siye Tusikione??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kipi wakionacho wao Siye Tusikione???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Nov 9, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mimi kwa muda mrefu sasa nimekua nikijiuliza ni kitugani mashirika ya Fedha na Nchi za magaharibi wakionacho Tanzania na sisi hatukioni, Mh. Jakaya Mrisho kikwete alipo kwenda Marekani hivi karibuni alipewa tuzo na hizo tuzo, moja wapo ikiwa ya Utawala bora, na kuna ripoti mbalimbali zimekua zikitoka za kuisifia Tanzania kuwa imepiga hatua kwa mambo mengi, ikiwemo hili swala la Utawala bora na kukuza uchumi, wakisema uchumi unakua kwa asilimia sita na point kadhaa, najuzi Pinda alipo kuwa akihojiwa Star Tv alisema Tanzania ni moja kati ya nchi kumi barani Afrika ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana na yeye anasema hii ni kwa mujibu wa Tafiti zilizofanywa na hayo mashiriki ya Kimagharibi.

  Sasa,. ndugu zangu mimi ninacho jiuliza huo utafiti unafamyikaje ili hali kila kukicha Watanzania ambao inabidi tufurahie ukuwaji wa uchumi tunazidi kuumia zaidi?, maisha yamekua magumu bidhaa muhimu kama chakula bei juu, polisi wanawanyanyasa raia bado, haki za wanyonge bado ni kitendawili, Kesi zinapigwa dana dana mahakani, hapa utawala bora na ukuwaji wa kiuchumi uko wapi na mimi sasa na shawishika kuuliza "NI KIPU HASA WAKIONACHO WAO HAO WA MAGHARIBI AMBACHO SISI HATUKIONI?" Naomba mnisaidieni kwa hili ndugu zangu.
   
Loading...