Ni kipi unajivunia kuwa Mtanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kipi unajivunia kuwa Mtanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Sep 12, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watz tuna safari ndefu sana kuelekea kufika kule tunakotaka. Kwanza, hakuna nia ya dhati ya kutaka kutekeleza kwa vitendo kauli zetu. Hili linajirudia mara kwa mara katika utendaji wa viongozi serikalini na hata katika taassisi zake. Tumekuwa watu wa kuongea tu bila ya kuwa na strategies of implementing what we say. Yaani kila kitu kimekuwa politicized. Hakuna hata sekta moja ambayo tunajivunia kuwa tumepiga hatua na sasa tunaweza kufikiria mambo mengine. Bada tuna lalamika na barabara, bado tuna lia shida ya maji nchi nzima, bado tunalia wodi na vitanda mawodini havitoshi, bado tunalia ubora wa elimu ni duni na watoto wanahitimu elimu ya msingi hawajui kusoma wala kuandika lakini wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza. Bado tunalia maliasili hazitunufaishi, tanzanite, dhahabu, almasi, shaba, makaa ya mawe, gesi na mafuta vyote vipo, lakini umaskini unaongezeka kila siku. Bunge letu limejikita kupitisha bajeti yenye nyongeza za kodi kwenye bia na soda.

  Serikali imefilisika kimawazo na hakuna ubunifu wa miradi ambayo italiongezea taifa mapato ya ndani. Hatuna viwanda vya ndani vya kutengeneza nguo, pamba kanda ya ziwa inadoda, hakuna wanunuzi, wanaonunua wanajipangia bei kana kwamba walilima wao. Wakulima wa tumbaku huku Mpanda hawajalipwa, tangu walianza kulima tumbaku mwaka jana mwezi wa tisa, hadi mwezi wa tisa mwaka huu wameanza msimu mpya wa kilimo, fedha za soko la tumbaku ya mwaka jana hawajaipata.

  Ni kipi tunajivunia kama watz? JK anazindua vyuo vikuu vipya, lakini nani atafika kusoma huko? Masharti ya mikopo yamekuwa magumu, watoto wa masikini lini watafika chuo kikuu? Shule za sekondari ambazo zilikuwa zinafaulisha watoto kwenda advanced level, zilipewa hadhi ya kuwa za A LEVEL tu, lakini leo hii shule kama MPANDA GIRLS imebaki na wanafunzi mia mbili tu wa advance, wengin wanahama na wengine hawaripoti kabisa.

  Shule haina waalimu, miundombinu mibovu, imefikia hatua mkuu wa shule ameomba halmashauri impelekee watoto wa O level, maana madarasa na mabweni ni matupu. Nini serikali inafanya?
  Kilimo kwanza kimeshindwa vibaya, pembejeo ni ghali sana, mvua zenyewe hazitabiriki hata kidogo, japo kuwa tumezungukwa na vyanzo vya maji kila mahali, lakini bado tunategemea mvua za Mungu ilihali tunakata miti na kuchoma mkaa kila siku. Ni miti mingapi inakatwa kwa ajli ya mkaa Tz nzima kwa siku? Lakini bado serikali inatuaminisha kuwa mvua itanyesha na tuendeleze sera za kilimo kwanza. Sote tunajua, sehemu ambayo haina miti, hakuna mvua kabisa au kuna mvua za kusua sua, na kila siku miti inakwisha, serikali haina njia mbadala ya kuwafanya watz watoke kwenye matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda misitu iliyopo kwa ajili ya kuendelea kupata mvua, umeme na gesi ambavyo vingelitumika kama nishati mbadala ya kupikia, ni ghali sana, na wengi hatuwezi kumudu. Kipi tunajivunia?

  Maji ya ziwa Tanganyika, mto malagalasi, mto pangani, bahari ya hindi, ziwa victoria, ziwa nyasa (Japo wamalawi wanalitaka lote), ziwa rukwa na mito na mabwawa chungu zima vingeweza kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuondoa utegemezi wa mvua na watu wangezalisha mazao ya chakula na biashara mwaka mzima, umasikini ungelipungua kwa kiasi kikubwa, lakini wapi, ni aibu sana nchi kama JAPAN ambayo inaingia tz kama mara kumi kutuuzia mchele ilihali tuna mabonde mengi sana ya kulima mpunga karibu kila kona ya nchi hii. Eti, mwenzangu unajivunia nini kuwa Mtz?

  Hifadhi za taifa zenyewe zimegawanywa kwenye vitalu, vitalu vinamilikiwa na viongozi na/au wafuasi wao. vitalu vingine vimeuzwa kwa wazungu kwa ajili ya uwindaji na utoroshaji wa wanyama wetu. Ndani ya hifadhi, (kwa mfano Katavi National Park) kuna camp site, ambazo wazungu wanazimiliki na wao ndio wenye dhamana ya kuleta wageni kutoka katika nchi zao na wao wanalipa vikodi kiduchu katika hifadhi zetu. Lini hifadhi hizi zitajiendesha? Huko kwenye camp site, haruhusiwi mtu yoyote kuingia, imefikia hatua kuna viwanja vya ndege, kinachoingia na kutoka katika camp site hizo. Watu wanabeba madini, pembe za ndovu, ngozi za simba na chui kinyume cha taratibu. Tunajivunia nini katika nchi yetu?

  Uongozi umeoza. Hakuna uwajibikaji. Ni kama familia ya kambare, baba ana ndevu, mama ana ndevu, mtoto na waijukuu wote wana ndevu, huwezi kutofautisha baba wala mkuu wa kaya ni nani. Kuanzia kwenye Urais hadi udiwani, hakuna ambaye anaweza kumuwajibisha mwenzake. kila mtu ana mamlaka katika eneo lake, na mamlaka hayo, hayaingiliwi na mwingine. Matukio makubwa ya mauaji yanatokea katika nchi, lakini mkuu wa kaya kama hayupo vile, eti ni upepo tu, utapita. Nchi ni kama haina mtendaji mkuu wa serikali, Pinda hayupo, Kikwete yuko ughaibuni kila siku, sijui lini Kibaki alikuwa na ziara ya kiserikali nje ya nchi? Hata Sina kumbukumbu, pengine kwa sababu niko pembezoni mwa nchi.

  Rushwa imetamalaki kila idara ya serikali na chama tawala. Tumeshuhudia juzi hapa kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya mpanda, fedha zilitolewa kuhongwa wajumbe kana kwamba ni uchaguzi mkuu. Lini ccm watasimamia maneno yao? Lini takukuru watakuwa na meno ya kutafuna waliowaweka kwenye madaraka? Lini bias itaisha katika nchi hii kutoka kwenye vyombo vya dola? Watendaji wote wa serikali wako bize na harakati za kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 kana kwamba huu ni mwezi wa sita 2015. Kila mmoja yupo ki maslahi zaidi, minyukano kila kona na vijembe visivyoisha. Eti, ni kipi unajivunia kuwa mtz?

  Hata baada ya miaka 50 ya uhuru, bado watz zaidi ya % 70 wanafikiria watakula nini leo. Maendeleo yanayosemwa kwenye tafiti mbali mbali na kwenye utekelezaji wa ilani ya ccm hayaendani na hali halisi vijijinina mijini. Hali ni mbaya sana vijijini. Watu wanaishi kwenye makazi mabovu, miundo mbinu ni mibaya, mavazi ya hovyo, chakula kibovu, kifupi, watu ni maskini sana. Bei za vifaa vya ujenzi inazidi kupanda, cement, bati, nondo, rangi, misumali havishikiki, lini watu wataishi maisha bora? Lini watu wataishi kwenye nyumba za bati zenye sakafu? Hadi leo hii naandika waraka huu, watu hawajawahi kulalia kitanda chenye godoro. Ni tz hii hii. Watu wanalalia vilago (Misengele) vinavyotengenezwa kwa matete yanayomea kando ya maji. Mtu akiamka asubuhi anaondoka na mistari ya mtete kwenye uso na sehemu nyingiine za mwili wake. Ni Tz hii ambayo rais kila siku anazurura kuomba misaada ya maendeleo. Ni nchi hii ambayo rais anasafiri na msafara wa watu zaidi ya hamsini kwenda nje ya nchi. Ni nchi hii ambayo rais anatumia zaidi ya Tsh. mil. 200 kwenye safari yake moja, lakini wananchi wake, bado wanawaza watakula nini leo. Aibu sana. Sijui hata nijivunie nini kuwa Mtz.

  Yaani wtz tulio wengi tumekuwa kama vichaa, tunatembea tunaongea wenyewe barabarani, tunawaza kila siku tunaona afadhali ya jana, hakuna unafuu wa maisha japokuwa nchi yetu ina kila neema ya raslimali na utajiri mkubwa. Tunaishi kifukara na kimaskini katika nchi tajiri. Maisha ni magumu hata hayasimuliki. Juzi nimepita kwenye kijiji kimoja hapa Mpanda kinaitwa Kasokola, kulikuwa na mkutano wa kukusanya maoni ya katiba mpya. Japokuwa kijiji kina wakazi wengi sana, lakini waliohudhuria kwenye mkutano walikuwa wachache sana. Nilipata fursa ya kuongea wachache ambao walikuwa bize na shughuli zao kando tu ya mkutano. Niliwauliza kwa nini hawatoi maoni yao ya katiba mpya? Majibu niliyoyapata. "Katiba nini? Hapa nilipo hata sijui jioni nitakula nini, halafu nikapoteze muda kuongea kitu ambacho kitawapa wengine chakula na maisha mazuri?" Watu wamekata tamaa, hata hawana muda wa kushiriki kwenye mambo ya msingi ya Taifa kwa sababu tu hawajui nn watakula. Hakuna kitu kibaya kama njaa. Huwa tunapata mawazo ya kujenga, kuvaa vizuri, kununua magari na kujenga maghorofa, baada ya kushiba. Kama mtu una njaa, wazo pekee linalokuwa kichwani ni "Wapi nitapata chakula." Kama serikali yetu hata baada ya miaka 50 ya kuwa huru imeshindwa kuwahakikishia wananchi chakula cha uhakika, nini imeweza? Maana mahitaji ya msingi ya binadamu (Human basic needs) ni chakula, mavazi na malazi. Vyote hivi, bado ni tatizo kwa Mtz wa kawaida. Chakula ni issue, mavazi usiseme, ni aibu tupu, malazi ndiyo hayo, ukiiona nyumba tu kwa nje, unajua humo ndani hakuna kitanda wala godoro, watu wanajifunika kanga, hata shuka hakuna. Ni nini unajivunia kuwa mtz?

  Mimi binafsi kama STK ONE, kutokana na aina ya maisha ambayo ninaishi na maisha ya watu ambao wananizunguka, kweli kutoka moyoni kabisa, sina ambacho naweza kujivunia kama Mtz. Sijui wewe mwana JF mwenzangu, unajivunia nini kama MTANZANIA?

  STK ONE, KATAVI.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Bla bla nyingi halafu hakuna chochote cha maana.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Najivunia utaifa wangu hata kama nchi iko kwenye autopilot. Naamini kwa raslimali tulizo nazo kuna siku tutaikomboa na kuifadi. Kwangu Tanzania ni mtaji kuliko kitu chochote. Sina mawazo ya kukata tamaa ya kuiangalia Tanzania kwa macho na mtazamo wa leo. Kuna siku tutaikomboa Tanzania na kuifanya yetu na kuifaidi.
   
 5. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Najivitia uhuru nilionao wa kuwa mtanzania kwa kuzaliwa na kwamba ninaendelea kuamua nani awe kiongozi wangu bila shuruti. Viongozi wetu wanatokana na sisi na ni sisi tunaowachagua. Kama ni wabovu basi wanaowachagua ndio wabovu zaidi!
   
Loading...