Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukiwa umefulia ambayo leo ukiikumbuka unacheka tu?

Hela anapata mikoba(kondakta) mimi ilibidi niwe kimakakati sana. Ikifika saa 4 natoa buku 5 naweka kwenye kamfuko ka jeans kale kadogo. Saa 10 naweka tano tena. So jioni kwenye mgao wa posho nakuwa nmemtangulia dereva kwa 10,000. Nakama unavyojua kwenye mgao kondakta anapata kidogo na dereva anapata hela nyingi zaidi. Yaani kama baada ya kujaza mafuta na kutoa malengo ya boss mkabakiwa na 50,000 inamaana dereva 30,000 na kondakta 20.
Siku nzuri ilikuwa mkipata watu wa kukodisha kwenye harusi mnapata hela nyingi sana coz mnatumia mafuta kidogo,mnalipwa kibunda,mnapata msosi wa bure na ndio mnapata muda wa kulala sana.
Kipindi hicho ndio nilielewa thamani ya usingiz yaaani. Nalijizoelea mkoani kwetu kuamka saa 1 au 2 sikuwa kuelewa kwanini binadamu anaamka saa 10 alfajiri. Ilikuwa nikipata nafasi ya kulala aiseee nilichagua kulala kuliko kula
 
Ukipata muda wa kulala unakimbia Mwendo wa ngiri mkia juu
 
Kwenye kazi hii makondakta ndio wana afadhali, na asilimia kibwa ni wezi vibaya mno! Na hata ukifuatilia kwa ukaribu maisha ya dereva wa daladala na kondakta ni tofauti sana! Ile kazi ni kama imelaaniwa! Na bahati mbaya maboss hawawaelewi madereva kwa makosa ya kondakta.

Makondakta kila siku wanakimbia na pesa za watu, si hesabu si mafuta sio posho ni mtihani sana
 
Huo mziki wa kuamka kabla raia hawajaamka na mda wa kupaki wewe unaenda kupaki, huku wale raia uliokua umeamka kabla yao nao wameshaenda kulala



Mara ya mwisho nimuambia boss, ukitaka niamshe hii gari unigee na kitabu chenye namba za simu za abiria, maana kuna muda unatafuta abiria mpaka akili zina hama, inakubidi uwauze hata wale uliokua nao ukaanze upya


Abiria wengine wanadharau balaa wanaona wanaofanya ile kazi ni kama walisha potea humu duniani, kua hawana wanalolijua chini ya jua na wamesha feli kimaisha, pyschology hii ilikua inaniumiza sana, mtu kunichukulia anavyojisikia yeye


Kingine kilichokua kinanitatiza, ukichukua gari ya hesabu 100,000 na ukichukua gari ya hesabu 90,000 au 80,000 au 70,000 utashangaa posho ni ilele, hapo ndipo ninapochokaga
 
Ufunuo mstari wa ngapi jombaaa
 
Chai hii mbona imepoa sana jamaniq1q
 
.......Nimekumbuka kipindi tunavunja neno kuvunja wenzangu (wauza mitumba wana ni elewa) Tulikua tuna vunja ma balow ya mtumba na kupiga mnada Kwa ma pointer.......

.........Majumba ya Godoro Yana rushwa huku na Kule chap chap Mimi NDIO mkusanya pesa utajua hujui.......

.......Hapo ndipo niliweza kuiheshimu Kaz ya kondakta wa daladala tena iwe Incher milango miwili...

🥴😳😳😀😊😊🤓🤓
 
Hii kazi niliifanya morogoro kule mvua wilayani walikua wanajenga hospital ya wilaya dadeki kazi sikua na uzoefu nayo afu nasaidia mafundi watatu asee sitokaa nisahau huu msoto kila siku nikikua nasema kesho sirudi ila kukikucha nakaza roho nilikomaa hadi nikafikisha 400000 japo pesa nyingine nilidhurumiwa na jamaa anaitwa Benjamin.

Mi pale nilienda kwa lengo la kupata pesa ya kodi niliyokua nadaiwa pamoja na madeni.

Ila nilikua nashangaa majamaa yanavyopeana connection za kazi za ujenzi najiuliza hivi hawa jamaa wanapumzika lini.
 
 
 
Daaah interesting story
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…