Ni kawaida shingo ya mtoto wa miezi minne kuwa haijakaza?

Umeolewa? Kama una mme huo ni uzembe wenu wa kumfanya mtoto a chelewe kukomaa. Mwanangu miezi miwili na nusu lakini shingo ilisha kaza kitaambo
Mkuu naona kama umekurupuka hivi,rejea thread mtoto aliumwa siku mbili baada ya kuzaliwa,halaf mim ni me
 
Habari zenu wanajamvi,

Naomba kueleweshwa kitu, mwanangu ana miezi minne toka kuzaliwa lakini mpaka sasa shingo yake haijakaza je ni kawaida au? Lakini ni mchangamfu sana yuko vizuri ni hilo la shingo tu.

NB: Alipozaliwa aliugua yellow fever akakaa chumba cha joto kwa siku 10, then akaruhusiwa. Je inaweza ikawa imechangia kitu?

Nawasilisha kwenu kwa ushauri asante
Kwa kawaida watoto wengi huwa wanakuwa wamekaza shingo katika umri wa miezi minne.

Ndiyo, manjano (neonatal jaundice) inachangia mtoto kuchelewa kukaza shingo.

Inategemea manjano yake ilikuwa kiasi gani

kwa case yako inaonekana ilikuwa kali na kwa muda mrefu hadi akahitaji tiba ya mwanga (phototherapy) kwa siku 10.

Ni vyema ukawafika hospitali ya uhakika anatakiwa apewe msaada wa tiba ya mazoezi (physiotherapy) aweze kufikia hizo hatua
 
Umeolewa? Kama una mme huo ni uzembe wenu wa kumfanya mtoto a chelewe kukomaa. Mwanangu miezi miwili na nusu lakini shingo ilisha kaza kitaambo

Mkuu watoto wakizaliwa wanaweza kutofautiana ukuaji kutokana na sababu mbalimbali, kama wako shingo imekaza miezi miwili na nusu haimaanishi kila mtoto shingo yake itakaza wakati huo, kwa hiyo huna haja ya kumlaumu mtoa mada ila ni vyema ungempa mawazo afanye nini kama unahisi mtoto wake kachelewa kuliko kawaida.
 
Kabla ya vote je umejaribu kumkalisha at least sekunde tano? kama analia sana,na hakai jitahidi kuwa karibu na daktar hilo tatizo lilishatokea kwenye familia yetu kama halii na anakaa kidogo itakuwa ni unene
Ulitumia tiba gani asee
 
Vip dada naona ni Muda mrefu Sasa mtoto wako alikuja kuwa sawa maana hata wa kwangu yupo hivyo na aliugua manjano akakaa kwenye mwanga siku 10 ila mpaka sasa hajakaza shingo miez 6 Sasa
 
Back
Top Bottom