Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
"Wana macho lakini hawaoni" - Ni nukuu maarufu iliyopo katika vitabu mbalimbali vya dini, ipo katika Biblia na ipo katika Quran. Kwenye Biblia nukuu hiyo imetajwa maeneo mengi kama vile Mathayo 13, Ezekieli 12 n.k.....Kimsingi nukuu hii inawazungumzia BINADAMU ambao huwa HAWAFIKIRI sawasawa, binadamu waliofungwa fikra zao.
Kwa kuwa hii ni thread yangu kwa mwaka huu, na kwa kuwa nimekuwa kimya katika jukwaa hili kwa takribani miezi 3, shule imekaba kidogo. Naomba niitumie thread hii kutoa salamu zangu za heri ya mwaka mpya kwa wana jamvi wote na pia kutoa pole kwa Makamanda kwa kumpoteza mpambanaji muhimu ambaye KUBENEA anadai AMEJITEKA, rafiki yangu Bernard Rabiu Saanane.
Mwaka 2015 niliwahi kuandika CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi na baadae mwezi wa nane mwaka jana 2016 nikaandika tena Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi leo kwa mara nyingine tena nalazimika kuandika mfano wa maneno hayo, hasa baada ya kusoma kilichoandikwa na Mhe Mbunge John Heche jana na baadae Mtatiro leo asubuhi. NI WAZI MANENO YAO YANDHIHIRISHA KUWA UPINZANI WA NCHI YETU UNA OMBWE KUBWA LA UONGOZI.
Ni ujinga tena upumbavu uliokomaa ambao wajuzi wa mambo wanaita "umbumbumbu" kwa wapinzani kuendelea kuvinyooshea kidole vyombo vya dola kila baada ya kushindwa uchaguzi.
MWENYEKITI Mtatiro anaposema CCM inaitumia DOLA, inatumia NEC, inatumia Rushwa, inatumia Hila, inatumia Mabavu wakati tunajua kuwa Mgombea wa CUF jimbo la Dimani hata fomu yake iliyopelekwa NEC haijapita kwenye ofisi ya Mwenyekiti wake, yaani kwa mgogoro mliouasisi wenyewe, mkaupalilia na kuuwekea mbolea kisha leo mgombea wenu anaposhindwa, bila aibu, bila hata soni unatoka mbele ya umma kusema umeshindwa uchaguzi kwa hila na kwa kuwa CCM inatumia Dola na kwamba NEC inatumika...tafadhali sana acha UJINGA wa namna hii. Ni kweli CUF ilitegemea USHINDI...seriously kabisa..???
Lakini ukweli ambao mmeendelea kuupuuza ni ule unaoendelea kudhihirika kuwa WATANZANIA sio WAJINGA...mlisimama na kumnadi Lowassa kuwa ni mwizi katika kila kona ya Nchi hii, leo ndio anasimama kwenye kila jukwaa lenu akinadi wagombea wenu wa Ubunge na Udiwani, na kila alipokanyaga Lowasa kwenye Kampeni mmeshindwa...mnasema CCM inatumia Dola...Watanzania sio wajinga.
Kimsingi Umaarufu wa UFIPA umepungua..,leo haitajwi tena UFIPA, inatajwa Lumumba, Haitajwi tena CHADEMA anatajwa LOWASSA, mmeendelea kumnawirisha mtu badala ya Chama, leo Mbowe hasikiki, Katibu Mkuu Mashinji ndio kabisa kama vile ni mfu, BAVICHA wanagombana na Vodacom na wanaidai Serikali iwarudishie Ben Saanane akiwa HAI tena asiwe hata na uvimbe wala mchubuko....then mnataka kushinda uchaguzi,,,HOW..? Hakuna hata hoja moja ya Wananchi mnayoisimamia, sio Rushwa, sio Ajira, sio Huduma za Maji, sio Umeme, sio Miundombinu, sio Bei za Vyakula/Mazao. CCM wanao ujasiri wa kutaja rushwa, wanaujasiri wa kuzungumzia maji, Waziri wa CCM anasema kuhusu bei ya Umeme, Rais anayetokana na CCM anaitengeneza upya TANESCO, CCM inawaneemesha wakulima kwa bei za mazao kupanda (kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Nchi hii Korosho imeuzwa kufikia 5000 kwa kilo.)
Mnaposimamia na kupigania mambo ya kipuuzi kwenye mitandao na magazeti na kuyaacha mambo ya msingi, WANANCHI nao wanawaonesheni Upuuzi unaolingana na ule mliowaonesha.
Samahani sana nimetumia lugha kali kidogo, lakini ndivyo ilivyo Ujinga wa Mwafrika bila kiboko hautoki kirahisi..!!