Ni jambo jema kumshukuru Mungu

Ni jambo jema kumshukuru Mungu

thomas_360

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
1,458
Reaction score
1,436
Napenda kutanguliza shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kuweza kunipa pumzi ya uhai mpaka dakika hii, kuna waliotamani kuiona siku ya leo ila kwa neema yake wametangulia mbele za haki.

Napenda kutanguliza shukrani kwa kuweza kunipigania tangu naanza chuo mpaka nahitimu, haikuwa kazi rahisi ila yote ni kwa neema yake.

Hivyo napenda kuwaomba wadogo zangu, ndugu zangu ambao mwaka huu mnaingia mwaka wa kwanza, kwa wale waliobahatika kupata fursa hiyo basi ni vyema kumshukuru mungu iwe kwa ngazi ya Certificate, Diploma au Degree.

lakini pia Pia nawasihi mtumie fursa hiyo mliopata vizuri, muweze kuitendea haki na kuipigania. Usidharau kitu katika kusoma kwako kila kitu kichukilie kama chalenge katika mafanikio yako...siku zote tambua kuwa kuteleza sio kuanguka, hivyo basi pale unapoteleza hebu nyanyuka na ujipange upya.

Pia kwa wale ndugu zangu ambao wamefanikiwa kupata mkopo mwaka huu, tusishangilie sana bali tumshukuru Mungu kwa yote yaliyotendeka, lakini pia kwa wale ambao hawajabahatika kupata huo mkopo hebu tusikate tamaa kila jambo huwa linatendeka for reason...ila kwa wale waliopata mkopo siwezi kuwashauri namna ya kutumia mkopo wako bali ni jukumu lako kuamua namna utakavyolitumia maana wakati ukifika wa kulirudisha utapambana na hali yako kulirudisha ili na wengine wanufaike pie..

Kwa wale ndugu zangu tunaendelea na masomo hebu tujitizame tilipotoka na tunapoelekea kimasomo kama maendeleo yako sio mazuri hebu jaribu kujipanga kwa mwaka huu uongeze bidii..kudisco kwa mtu chuoni huja automatic na usipojipanga mapema utakuja kujutia..inauma sana mtu kudisco ukiwa mwaka wa kwanza au wa tatu...nina mifano hai na inaniuma sana..na wimbi kubwa la watu huwa wanadisco miaka hiyo kwa program za miaka mitatu...

Then kwa wale ambao tumehitimu mwaka huu na ambao tayari wapo kitaa tusikate tamaa kama bado hatujapata channel za maana ipo siku naamini tutakula matunda ya miche tuliyoipanda....nashukuru sana kwa wewe uliyeweza kusoma ujumbe huu na kama unachochote basi tusaidiane hii ni Tanzania yetu na sisi ndo Watanzania wenyewe...
 
We acha tu mkopo sina APA nawaza mwakan niombe upya na chuo nakiona kileee kinaniacha ,,,uchungu nilionao nizaidi ya kifo mungu ananiona ...sijui nilimkosea nin ....udsm ileee sijui mwakan ntaiona tena
 
MUNGU akutangulie lakini Mimi ndo mwaka WA kwanza nahitaji ushauri wako zaidi
sijui unasoma program gani ila cha msingi usichukulie mambo ni marahisi...fuata ratiba za lectures na uhudhurie kuna issue za quiz ambazo huwa zinaweza kukufanya ukadisco.. discussion ni muhimu kama huwezi kujisomea muda mwingi maana watu tunatofautiana..Lakini pia kuwa huru kuuliza maswali usiogope kuchekwa au watu kufikiria swali lako halina maana...Chuoni kukesha ni mbwenbwe tu..cha msingi weka ratiba yako ya kujisomea vizuri ambayo haitokuhitaji kukesha.. Elimu ya Chuo ukiwa smart huwezi kuteseka kama watu wanavyofikiria..kwa life yangu ya kusoma chuoni sijawahi kusoma zaidi ya Saa tano...ukichoka kusoma usijilazimishe angalia movie kama ww ni mpenzi wa movie au kusikiliza muziki au kama ni mpenzi wa viwanja unaenda unajirusha kurefresh mind yako..maana kila mmoja anamna ya kupumzisha akili yake so ww utaangalia starehe yako ipo wapi..cha msingi tu usitumie muda mwingi katika maeneo hayo...
 
We acha tu mkopo sina APA nawaza mwakan niombe upya na chuo nakiona kileee kinaniacha ,,,uchungu nilionao nizaidi ya kifo mungu ananiona ...sijui nilimkosea nin ....udsm ileee sijui mwakan ntaiona tena
pole isee..ila usikate tamaa yote ni mapito na yana mwisho wake..usikae kujilaumu wala kuhisi umemkosea Mungu kwa jinsi unavyofikiria, Duniani hapa hakuna ambaye hajamkosea Mungu ila tu ni majaribu ambayo tunayapitia na hatupaswi kutetereka..ni kusimama na kuwa imara..kaa chini fikiria vizuri utapata majibu chanya yatakayokusaidia hapo mbeleni
 
pole isee..ila usikate tamaa yote ni mapito na yana mwisho wake..usikae kujilaumu wala kuhisi umemkosea Mungu kwa jinsi unavyofikiria, Duniani hapa hakuna ambaye hajamkosea Mungu ila tu ni majaribu ambayo tunayapitia na hatupaswi kutetereka..ni kusimama na kuwa imara..kaa chini fikiria vizuri utapata majibu chanya yatakayokusaidia hapo mbeleni
Asante mkuu ....huu mwaka wangu yameshanikuta tayari sina namna
 
Back
Top Bottom