Ni ipi faida ya ndoa ukitoa watoto

Ni ipi faida ya ndoa ukitoa watoto

momara

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
463
Reaction score
491
Kama ambavyo kichwa cha habari kinajieleza. Kumekuwa na wimbi kubwa la wake kwa waume wote wakilalama juu ya kukosa furaha na faraja ktk ndoa zao.

Imefika hatua aliyeoa anajuta kwanini alioa na alieolewa pia hivyo hivyo. Na matatizo ni yale yale usaliti, kutokusikilizana, kutokupeana thamani, mazoea ndani ya ndoa, ubinafsi na mengine mengi.

Imefikia hatua uvumilivu ndani ya ndoa isiyo na furaha huletwa na watoto. Watoto wangu wataishi vipi ikiwa ndoa hii itavunjika ndio swali huja kichwani na mtu huamua tu kuvumilia.

Pia wako ambao huamua kuoa ili tu apate watoto ktk mtiririko unaoeleweka kuliko kuzaa na huyu mara yule kuepusha mgawanyiko wa watoto na kujenga familia isiyo umoja.

Na hapa nauliza tu kwa wanandoa mlio ndoani je ni ipi faida ya kuoa ukiondoa watoto?
 
Faida ya Ndoa nje ya watoto na sex ni kusaidiana majukumu na kufarijiana
 
Back
Top Bottom