Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,322
Mwaka 2013 nilipata fursa ya kushiriki kwenye mradi ulionisaidia kuitembelea Tanzania kwa 80%. Katika mradi huu nilifanikiwa kujiongezea marafiki wengi karibu kila pembe ya nchi. Kinachoendelea kunishangaza ni kuona marafiki wengi niliovuna maeneo mengi ya pembezoni na hasa "bara" wamekuwa ni waaminifu na wakweli kweli kweli.
Tunashirikishana kwa wengi kijamii na kiuchumi. Wengine sijabahatika kuonana nao tena lakini kwa njia ya mawasiriano tumekuwa wamoja na kwa hakika tumeweza ku"share value zetu " na kusonga kwa kila mmoja kufikia malengo.
Tatizo limekuwa kwa wale niofahamiana nao Dar, sio wote lakini wengi wao wanaonekana si watu wenye utu.
Ubabaishaji umewajaa na kujikweza kwingi. Wanaishi kwa hisia na mihemko zaidi kuliko uhalisia. Nimekaa nikajiuliza hivi kumbe ukiishi Dar jiji linakubadili kutoka mtu mwenye utu na kuwa mtu mwenye kupenda kidogo kitu zaidi ya utu. Pengine wana jamvi hebu semeni neno katika hili.
Ni hisia zangu au lina ukweli