Ni heri tatizo liishie kwako, kuliko kulipatiliza kwa vizazi vyako

Misunderstood

JF-Expert Member
Aug 4, 2020
384
882
Binadamu wengi duniani tunapitia matatizo mengi bila kusahau la umasikini. Dunia imejaa taabu, shida, majuto nk. Wengi wetu hasa jamii zetu za kiafrika ishu za uchawi, kulogana zimekithiri.

Bado hujahangaikia tumbo na hapo ukute huna mchongo wa kueleweka, kila siku unasikilizia.

Ya nini kuleta duniani viumbe visio na hatia? Viendeleze shida ulizonazo? Uwapatilize maroho uliyobeba kutoka vizazi vyenu? Au ndo akisoma aje kukusaidia?

Tuache ubinafsi jamani, tufikirie sana kabla hatujaleta watoto katika hii dunia hasa ukiona maisha yako yenyewe ni ya taabu. Sio lazima kila mtu awe na mtoto.

Heri shida ziishie kwako ndugu! Hii dunia si lelemama, tutafakari hili jambo kiundani zaidi kila mmoja kwa wakati wake. Naweza nikawa sijaweka hoja nzito sana, ila ndani ya hichi nilichoandika kina ujumbe mzito na wa maana!
 
Kila mtoto uja na baraka zake ba unaweza kuanza vzuri kabsa ukawa na kila ktu cha kuitwa mzaz au kijana aliefanikiwa mpaka ukawa sample ya mfano mtaan au kijijn kwenu ila sku mambo ya kbadlka utamtaman ambae hakuwah kua nacho
 
Mwambie hayo maneno :-

1. Mwanamke mwenye 35 years na bado hajatoboa Kimaisha na hana Ndoa.

2. Mwanaume ambaye ana 40 na bado hajatoboa kimaisha na hana Ndoa.

3. Mwanamke wa Kijijini ambaye amefeli na kuishia Darasa la 7 huku wenzake wote wanaomzunguka wana watoto na wengine mpaka watoto wawili.

Kisha urudi uje utuambie wamepokeaje!?

Mtoto ni Faraja.
Mtoto ni Uhakika kwamba wewe sio Mgumba.
Mtoto ni Baraka.
Mtoto ni Zawadi kutoka kwa Mungu.
Mtoto ni Furaha kwenye Mahusiano.
Mtoto ni Mtoto.
 
Binadamu wengi duniani tunapitia matatizo mengi bila kusahau la umasikini. Dunia imejaa taabu, shida, majuto nk. Wengi wetu hasa jamii zetu za kiafrika ishu za uchawi, kulogana zimekithiri.

Bado hujahangaikia tumbo na hapo ukute huna mchongo wa kueleweka, kila siku unasikilizia.

Ya nini kuleta duniani viumbe visio na hatia? Viendeleze shida ulizonazo? Uwapatilize maroho uliyobeba kutoka vizazi vyenu? Au ndo akisoma aje kukusaidia?

Tuache ubinafsi jamani, tufikirie sana kabla hatujaleta watoto katika hii dunia hasa ukiona maisha yako yenyewe ni ya taabu. Sio lazima kila mtu awe na mtoto.

Heri shida ziishie kwako ndugu! Hii dunia si lelemama, tutafakari hili jambo kiundani zaidi kila mmoja kwa wakati wake. Naweza nikawa sijaweka hoja nzito sana, ila ndani ya hichi nilichoandika kina ujumbe mzito na wa maana!
Niliwaza hili nikiwa form two nikamwomba Mungu asinipe uzazi hapo baadae lakini nilipokua nikatamani watoto ikabidi nifunge kuomba ili kuvunja kiapo.Nina watoto wawili,Nina hasira sana twenyewe tuna hasira kama mbogo nawaombea waondolewe roho ya kukataliwa maana mama Yao ndoa ilishanishinda.Mungu awatetee wanangu
 
Mi mpaka nyumba iishe ndo natafuta mtoto na kuoa kabisa sitaki shida nimetokea kweny shida naelewa
Hapo kuna kabila ukifa hivyo wana kusweka Gunzi kwa Mku****u .
Wanamaanishi mtoto wao kafa lakini alikua ndio hivyo tena (sio Riziki)
 
Mwambie hayo maneno :-

1. Mwanamke mwenye 35 years na bado hajatoboa Kimaisha na hana Ndoa.

2. Mwanaume ambaye ana 40 na bado hajatoboa kimaisha na hana Ndoa.

3. Mwanamke wa Kijijini ambaye amefeli na kuishia Darasa la 7 huku wenzake wote wanaomzunguka wana watoto na wengine mpaka watoto wawili.

Kisha urudi uje utuambie wamepokeaje!?

Mtoto ni Faraja.
Mtoto ni Uhakika kwamba wewe sio Mgumba.
Mtoto ni Baraka.
Mtoto ni Zawadi kutoka kwa Mungu.
Mtoto ni Furaha kwenye Mahusiano.
Mtoto ni Mtoto.

Yani unazaa mtoto kwasababu atakuwa faraja katika shida unazopitia? Mtu masikini kwanini ulete watoto wateseke jamani
 
Umaanisha mwanaume mwenye miaka 40 hawezi kujilisha Wala kujivalisha? Huyu hastahili kuwa na familia kabisa Bora aachane na hizo habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani unazaa mtoto kwasababu atakuwa faraja katika shida unazopitia? Mtu masikini kwanini ulete watoto wateseke jamani
Mkuu Tafuta kwanza , shule, income, then ndio utafute familia, kama ukifikisha 40 huna mtoto ila una income na una huna uwezo wa kuzaa tena, unaweza ku adopt mtoto kutoka kwenye watoto yatima au ndugu...watu wanajua ku complicate things.
 
Fanya utanyavyo Ila usiache kujizaa, watoto wawili hawezi kukushinda Kama wewe ni Mchapakazi kweli.

Duniani tumekuja kuishi Kwa furaha na kuzaa.

Usizae watoto wengi Ila kamwe usiache kujizaa.

Kuzaliwa ni deni, kuzaa ni kulipa Deni.
Kama ulizaliwa lazima nawe uzae angalau mmoja kama haujao na Kama umeoa basi angalau wawili ili kuji-replace wewe na mkeo
 
Napingana na wewe, we zaa kadri ya mayai yako, KILA mtoto ana akili yake, sema hii ya kuzaa kama investment yaani unategemea mtoto ndo aje akusaidie ishapitwa na wakati.
 
Cha muhimu ni kubadili mind set wekeza kwenye kufikiri ambapo si lazima upite shule. Ukiwa na google ni phd tosha, KILA kitu kimo mle ni wewe kuperuzi tu. Wafunze ujasiliamali tangu wanazaliwa watatoka tu achana na njia ya shule watapoteza ramani ya maisha bure, shule wapite kama sehemu ya ukuaji tu na sio sehemu ya kuja kutokea. Njia ya vyeti ni bahati nasibu ktk maisha. Tumia njia za kichina, china wao awaamini njia ya vyeti wao wanaamini njia ya mkono Kazi.
 
Niliwaza hili nikiwa form two nikamwomba Mungu asinipe uzazi hapo baadae lakini nilipokua nikatamani watoto ikabidi nifunge kuomba ili kuvunja kiapo.Nina watoto wawili,Nina hasira sana twenyewe tuna hasira kama mbogo nawaombea waondolewe roho ya kukataliwa maana mama Yao ndoa ilishanishinda.Mungu awatetee wanangu
Pole sana inaonekana umepitia magumu sana huko nyuma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom