Ni halali kulipa madeni ya shule ya enzi za Kikwete ndani ya mfumo wa elimu bure?

UZZIMMA

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
410
477
Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda.

Enzi za Kikwete tulisoma elimu ya sekondari kwa pesa. Hii inajumuisha ada na michango mingine shuleni.

Kwa mfano mimi, kuna baadhi ya nyaraka kutoka shuleni sijachukua, ikiwemo "living certificate". Na wananizuia kuchukua hadi nilipe madeni ya shule.

Je ni halali kulipa hayo madeni au laa?
 
Enzi za Kikwete zimeshapita na watu wake. Kama wenzako walilipa wewe kwanini hukulipa? Ulikua unatumia huduma kwa pesa za wengine!

Nenda kalipe madeni ya watu, sera ya Elimu bila malipo haikuhusu wewe.

Ilianza mwaka jana 2016 kwa waliopo shuleni.
 
Mwenyezi Mungu awabariki na kuwalinda.

Enzi za Kikwete tulisoma elimu ya sekondari kwa pesa. Hii inajumuisha ada na michango mingine shuleni.

Kwa mfano mimi, kuna baadhi ya nyaraka kutoka shuleni sijachukua, ikiwemo "living certificate". Na wananizuia kuchukua hadi nilipe madeni ya shule.

Je ni halali kulipa hayo madeni au laa?


Duuh!!
 
Wewe living certificate itakusaidia nini?wakati kuna Result slip.au ulitaga ndo unataka kutumia iyo kuombea vibarua,Maana inaonekana umemaliza mudaa
Si mbaya kuwa nayo kwani hujui kesho kipi kitatamkwa
 
leaving certificate sio living mkuu,mi nadhani ni halali na ni sawa kulipa kwasababu kipind hcho huyo ndugu yako anasoma alitumia rasilimali za shule ambzo ilitakiwa gharama zake ziwe juu ya wew mzazi.ko ni sawa ufanye vema kulipa.
 
Wewe living certificate itakusaidia nini?wakati kuna Result slip.au ulitaga ndo unataka kutumia iyo kuombea vibarua,Maana inaonekana umemaliza mudaa

Japo umetoka nje ya lengo la uzi. Ila ni kweli nilitaga japo nilirudia mtihani baadaye nikafanikiwa!

Na leaving certificate nataka kukata cheti cha kuzaliwa. Cheti cha CSEE hawakihitaji.
 
Ahsanteni kwa mawazo na ushauri wenu. Sina budi kulipa hilo deni.
 
Na leaving certificate nataka kukata cheti cha kuzaliwa. Cheti cha CSEE hawakihitaji.[/QUOTE]
Hongera kwa juhudi ulizofanya.Kama unadaiwa pesa nyingi mtafute Mwalimu au sekretari wa headmaster then uongee nae kiutu uzima kwa kumpa pesa ya nyama,naamini atakupatia.
 
Katika sheria,kanuni moja ya msingi ni kwamba sheria haitumiki "retrospectively".

Yani, tukisema tunapitisha sheria kuanzia leo ni marufuku kuvaa shati la bluu,ukikamatwa utapigwa viboko kumi,hatuwezi kuja na picha umevaa shati la bluu juzi tukataka kukuchapa viboko kumi.

Kwa sababu muda wa sheria hiyo kuanza kutumika ulikuwa haujafika.

Vivyo hivyo kwako.

Hutakiwi kusamehewa deni kwa sababu muda wa kusoma "bure" ulikuwa haujafika.

Lipa deni tu.
 
Kwahiyo wadaiwa wa mikopo ya vyuo enzi ya kikwete ,mkapa wasilipe
 
Back
Top Bottom