Ni halali kuingilia ugomvi wa mke na mume

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Katika familia moja ya ndugu yangu,kuna ugomvi mkubwa umetokea

Katika mzozano huo wakaanza hadi kupigana ambapo mwanamke alianza kupiga kelele akiomba msaada kutokana na kipigo cha mmewe

Mwanaume jirani anafika,anataka kuamua ule ugomvi,lakini mume wa mwanamke anaanza kupigana na huyo mwanaume jirani yao kwa sababu ya hasira na kuingilia ugomvi

Mwanaume aliyekuja kusaidia anaona jamaa kama amehamishia hasira kwake,naye anaanza kujihami,anamkunja yule mwanaume na kipondo kikali anamzidi nguvu na kumkalia kifuani na kuanza kumniga

Mwanamke anaona kama mume wake anaumia,anamshika yule jirani amuache mumewe

Ugomvi unazidi na jamaa anazidi kumshambulia mumewe

Mwanamke anachukua kigoda anampiga kichwani yule mwanaume aliyekuja kusaidia hadi anazimia

Baadae watu wakawa wamesaidia pale na akarudisha fahamu na kumhoji,kwa nini uingilie ugomvi usiokuhusu hasa wa mke na mume

Kwani jaman ni vibaya kuamua ugomvi wa wanandoa
 
Ugomvi wa aina yeyote unatakiwa kumalizwa, kitu cha msingi angalia kama unawamudu wote ndio inapendeza zaidi, niliwahi kuamulia ugomvi walishikiana visu kabisa katika jitihada zangu za kuamlia nilianza na mwanamke mwenye kisu akapoteza fahamu chini mumewe kahamishia vita kwangu nae hakuchukua round.
 
Unaingilia lakini unaangalia kwanza unaweza kummudu huyo mtu kwanza...hahahahah ya nini kupigwa ukatolewa meno ukabaki kigego.. hahaahah
 
Katika familia moja ya ndugu yangu,kuna ugomvi mkubwa umetokea

Katika mzozano huo wakaanza hadi kupigana ambapo mwanamke alianza kupiga kelele akiomba msaada kutokana na kipigo cha mmewe

Mwanaume jirani anafika,anataka kuamua ule ugomvi,lakini mume wa mwanamke anaanza kupigana na huyo mwanaume jirani yao kwa sababu ya hasira na kuingilia ugomvi

Mwanaume aliyekuja kusaidia anaona jamaa kama amehamishia hasira kwake,naye anaanza kujihami,anamkunja yule mwanaume na kipondo kikali anamzidi nguvu na kumkalia kifuani na kuanza kumniga

Mwanamke anaona kama mume wake anaumia,anamshika yule jirani amuache mumewe

Ugomvi unazidi na jamaa anazidi kumshambulia mumewe

Mwanamke anachukua kigoda anampiga kichwani yule mwanaume aliyekuja kusaidia hadi anazimia

Baadae watu wakawa wamesaidia pale na akarudisha fahamu na kumhoji,kwa nini uingilie ugomvi usiokuhusu hasa wa mke na mume

Kwani jaman kwani kuamua ugomvi wa wanandoa
imagine umepanga nyumba moja na wanandoa fulani halafu siku unatokea ugomvi kati yao, unatokea kugombelezea,katika kuamua ugomvi inatokea bahati mbaya unapigwa jichoni unavimba.......afu kesho unaamka km kawaida unawasikia hao wanandoa wanacheka kuonyesha wamepatana.....Hii kitu inauma sana kwani waweza fikiri wanacheka na kukuteta wewe unweza dhani wanasema "baba Juma jamaa kaumuka" ugomvi wa wanandoa hapna ,nasema hapana...narudia tena hapana
 
cutelove huyo mwanamke kweli anampenda mumewe! Hii ni ishara ya upendo na baada ya hapa mkanye mwanaume ampende mkewe na asimpige tena
 
Ugomvi wa aina yeyote unatakiwa kumalizwa, kitu cha msingi angalia kama unawamudu wote ndio inapendeza zaidi, niliwahi kuamulia ugomvi walishikiana visu kabisa katika jitihada zangu za kuamlia nilianza na mwanamke mwenye kisu akapoteza fahamu chini mumewe kahamishia vita kwangu nae hakuchukua round.
Wew balaa
 
Kuamua ni busara..lakini usi-take side...
Wewe amua ugomvi wasiuane tu lakini usijifanye unajua kusolve migogolo.
 
imagine umepanga nyumba moja na wanandoa fulani halafu siku unatokea ugomvi kati yao, unatokea kugombelezea,katika kuamua ugomvi inatokea bahati mbaya unapigwa jichoni unavimba.......afu kesho unaamka km kawaida unawasikia hao wanandoa wanacheka kuonyesha wamepatana.....Hii kitu inauma sana kwani waweza fikiri wanacheka na kukuteta wewe unweza dhani wanasema "baba Juma jamaa kaumuka" ugomvi wa wanandoa hapna ,nasema hapana...narudia tena hapana
Ni kuwaacha watoane meno huko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom