Ni haki kwa muajiri kuwapa wafanyakazi mkataba wa mwaka mmoja kwa kazi endelevu?

Daliso

Member
Mar 29, 2017
46
30
Kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiono kazini kufungu cha kumi na nne kama kinavyoonekana hapo chini,

14.-(1) Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina zifuatazo-
(a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa;
(b) mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za
wataalamu na mameneja
(c) mkataba wa kazi maalumu
Je? ni haki kwa majiri wa Kitanzania kuwapa wafanyakazi wake mkataba wa mwaka mmoja mmoja kwa kazi ambazo ni endelevu
 
Mkuu umeuliza swali la jambo pinalonikabili,Nina miaka mitatu napewa mkataba wa mwaka mwaka na sasa kunafununu wanataka kuninyima mkataba mpya,
Wanasheria njooni mtusidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio mwanasheria mimi, ila kwa ninavyodhani inakubalika kisheria. especially kwa private firms. ulitaka wakupe mkataba wa miaka 10 mkuu?
ukiwa liability washindwe kuku-fire?
 
Back
Top Bottom