Ni haki kujiua au kuua kwa ajili ya mchepuko?

Wimsha

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
518
503
Hodi jamvini

Naomba ushauri wenu juu ya yatokanayo na mapenzi katika jamii yetu.
Juzi nilikuwa na wakati mgumu baada ya rafiki yangu wa karibu kuniletea nakala ya usia wa ?mali zake?. Yeye ni rafiki yangu wa karibu tumesoma wote sekondari na hata jeshini tulikuwa intake moja ?operesheni Nidhamu?.  Ni baba wa familia ya watoto watatu na ni mpenda dini kwelikweli.

Mwanzoni nilidhani kuwa ule usia ulikuwa kwa nia njema ya kuuhifadhi lakini wakati namsindikiza (alikataa mke wangu asimsindikize) ndipo akaniambia kuwa amefikia uamuzi wa kujiua au kuua au vyote viwili. Baada ya kumhoji akadai kuwa kuna mpenzi (Mchepuko) ambaye amemkataa na juhudi zote za kumrejesha kundini kushindikana.

Mwanzoni nilidharau lakini tone na muanekano wake uliashiria kuwa aliimaanisha alichokiamua. Baada ya kumhoji sana niliamua kumpigia mchepuko na kukubaliana kukutana siku ilele jioni maeneo ya Kijichi. Kilichojiri wakati wa mahojiano ni pamoja na mchepuko ?mchepuko ulikuja unadrive ingawa sikuona kadi ya gari ina jina gani? kutamka waziwazi kuwa uwezo wa jamaa kuhudumia umefika mwisho na hawezi tena kuendelea na uhusiano.

Sababu ya pili ni kwamba mke wa rafiki yangu alishahisi mahusiano yao jambo ambalo jamaa alikiri kuwa alishaulizwa sana juu ya hilo. Isitoshe mchepuko ulieleza wazi bila chenga kuwa sasa kafunguliwa biashara duka la nguo maeneo ya msasani na ndio sababu ya kuhama kijichi.

Baada ya mazungumzo marefu tulikubaliana tupeane muda kila mtu akatafakari tukutane jumapili.Najua huenda uamuzi huu ni temporary solution.

Nini kifanyike waungwana? Ni haki kutoa roho ya binadamu yeyote kwa ajili ya mapenzi?
 
mapenzi mapenzi haya.

mwambie asiwe lofa kiasi hicho. akijiua atapata nini sasa?
 
si haki ,, mwambie rafiki yako Mungu si baba yake .. aache ujinga unasema mshika dini ilihali anachepuka .. kiasi cha kukosa upendo na familia yake na aanaamua kujiua kisa mchepuko....

KABLA YA JUMAPILI MCHUKUE RAFIKI YAKO KAMPIME AKILI KUNA NYUZI ZIMEKATIKA
 
Ok, habari ni nzuri ila kichwa cha habari hakiko sawa.

Unauliza ni haki, haki kwa mujibu wa nini? sheria za nchi, za dini, utamaduni, jamii au ni haki kwa mujibu wa nini?

Kwa mujibu wa nafsi yako au nini?
 
Nawaza amekufa af mkewe analia aaah, plus nguo zake nyeupe mwenyewe, baadae anaitwa mjane wa fulani!!!!
mweeeeeee muwe mnawaonea huruma wawapendao
 
baba wa watoto watatu anataka kuwaacha watoto wake katika hali gani? sawa tunafariki kwa kua siku zetu za kuish duniani zimefikia tamati yeye anataka ajikatishe maisha kaambiwa kuzim kuna raha sana au vipi?? solution kuu ilikua abaki njia kuu mpeleke rafikiyo kwa wataalam wa saikolojia si akubali matokeo tu aangalie familia yake,msihi mpe maneno ya kiimani (kidini) penda sana kumtafuta kwa sim kila wakat ujue alipo na mwisho lililo kubwa akubali matokeo atulie na ndoa yake alee wanae.
 
mapenzi mapenzi haya.

mwambie asiwe lofa kiasi hicho. akijiua atapata nini sasa?

anakufa anaacha mchepuko unakula goodtime mjini mke Analia daily watoto na maisha magumu huu si upuuzi wa mwisho kabisa
 
Hao wataalamu wa saikologia wako wapi?
huko huko muishipo jaribu hata kuulizia au hata wewe unaweza mshauri jamaa aache haya mambo mshauri kwa uwezo wa mwisho kabisa muusie mtolee mifano watoto wanapokua na furaha pindi wamuonapo baba yao mke atakavopata tabu baadae na mchepuko utakavoish kwa raha ukiwa na uhakika wa kuendesha maisha yake huku yeye akiacha shida na mateso katika familia yake na wala asiue mtu yeye akubali matokeo kua hapendwi tu inatosha asonge mbele atulizane na ndoa yake.
 
anakufa anaacha mchepuko unakula goodtime mjini mke Analia daily watoto na maisha magumu huu si upuuzi wa mwisho kabisa

Ni upuuzi haswaa. .
Alitaka mchepuko abaki siku zote kwan amekuwa mke wake??
 
Huyo rafikio akili zake fyatu,huwezi kuwa na mke na watoto watatu halafu wazo la kujiua likakujia kichwani kwa tatizo lolote lile achilia mbali upuuzi uitwao mchepuko.Ile hisia tu ya simanzi na huzuni utakayoichia familia yako inatosha kabisa kufuta hilo wazo kichwani.
Kujiua ni aibu,ni hatia kwa sababu yoyote ile iwayo.
Halafu inashangaza kujua kwamba eti jamaa ni mshika dini!!!..
 
Back
Top Bottom