Ni Fani Inayopotea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Fani Inayopotea

Discussion in 'JF Doctor' started by Mkaa Mweupe, Jul 23, 2009.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanaJamii,

  Napenda kuwa silisha mada ambayo imenitatiza kwa muda sasa.

  Naona matangazo menengi ya biashara yanaanza kuharibu fani ya u-Dakitari. Nasema hivi nikiwa na maana ya kuwa, matangazo ya kisasa yanashawishi watu kutumia dawa bila ya kufanyiwa uchunguzi. Eti ukiwa na maumivu ya kichwa tumia... ukiona dalili za malaria tumia... sasa hapo ni kwamba kila mtu anakuwa ni dakitari binafsi lakini kuna magonjwa kama sukari ambayo dalili ni kama malaria.

  Wajameni fani yenu inapotelea wapi. Ni nini sauti ya ma-Dakitari itasikika dhidi ya matangazo kama haya au ndio segregation of duties ambayo madakitari mmekua ni wafamasia maana dili ni kuuza dawa na sio kusaidia kupata taifa lenye uhakika wa kuishi.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kweli haya matangazo yamekuwa too much.

  Mara sasa hivi kuna sijui Dawa tatu, Dawa mbili, na majina mengine kibaaao!
  Ila watumiaji wanaambiwa kuwa pale yakiwashinda, au maumivu yakizidi ndo wakimbilie kwa Daktari!

  Kama dawa hizo ni nzuri, kwanini kukesha kuzitangaza kwa nguvu hivyo?
  Kweli kuna kila sababu ya kuhoji uhalali wa dawa hizi, maana kinyume chake utakuta juhudi zote ZA kISERIKALI za kuondoa magonjwa sugu kama Malaria inakwamishwa na usugu unaoletwa na madawa haya ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kutosha kama ilivyo kwa Mseto na SP.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Mkuu, ila nadhani ni wahusika ni food and drug regulatory authority... ukiangalia fani ya afya, kuna nyanja maaluma zinahusika na masuala ya dawa na sifa zake ambao wengi wao si madaktari bali wagunduzi wa dawa na kemikali dakitari yeye ni mtoa tiba inayolingana na ugonjwa uliogunduliwa.
   
 4. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inaelekea Tanzania imefanywa ni uwanja wa majaribio. Enyi madakitari tuambieni kama ni kweli Chloroquine haitibu malari au ni janja ya nyani. Maana kama Kenya inaendelea kutumika iweje Tz. Au Tz wanadamu za tofauti.

  Ila la msingi katika hoja hii ni kwanini watu wanakosa imani na hawa madakitari na wauguzi? Je serikali inaliangalia vipi suala zima la afya ya wananchi wake?

  Maana majority ya waTz ni wale wenye uwezo mdogo, mfumuko wa maduka ya dawa baridi mitaani na matangazo yanayopotosha yanaiharibu jamii yetu.

  Ninakemea vitendo hivyo. Madakitari muache kuwa wafanya biashara.
   
Loading...