Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Huu ni muendelezo wa maigizo ya serikali ya Magufuli.
Mara tu baada ya baraza la mawaziri kutangazwa makamu wa rais mama Samia na Naibu waziri wa nishati na madini Dr. Kalemani walifanya ziara Geita katika kile kilichoonekana kama jitihada za kuifanya Geita kuwa ngome kubwa ya Magufuli.
Bahati nzuri na mimi nilikuwa geita.
Wakati wa hotuba zao, mama Samia aliwaahidi wachimbaji wadogo kupewa fursa ya ku~process magwangara (mawe yenye dhahabu kidogo) yanayotupwa na kampuni ya GGM ~jambo ambalo halijafanyika mpaka sasa, pamoja na kuwaruhusu kufanya kazi kwenye migodi iliyoshikiliwa na wawekezaji wakubwa kwa amuda mrefu bila kufanyiwa kazi.
Dr. Kalemani yeye aliipa kampuni ya buckreef muda wa siku 13 ili kuanza kazi lasivyo watanyang'anywa mgodi huo.Hili sihitaji kulieleza kwa undani sana kwa kuwa kuna mada hapa JF inayolihusu na iliyodadavuliwa kwa undani sana.
Basi, watu tukakaa macho juu maana hapa Geita hali ni mbaya sana na hilo eneo la stamiko lina dhahabu nyingi sana za juu.
kuanzia tarehe 20 wachimbaji wadogo wadogo wakingia kazini. Vijana wa kwanza kabisa ndani ya masaa 12 wakatoka na kilo ya dhahabu. Na wengine wakafuatia, shangwe ikataka kurudi Geita.
Sijui nini kikatokea ndugu zangu, kuanzia tarehe 24 FFU wakaingia Stamico na kuwaamshia vijana popo wa hatari (mabomu ya machozi na rungu za kufa mtu).
Sasa najaribu kujiuliza; kulikuwa na sababu gani kwa makamu wa rais na Dr. Kalemani kuwadanganya wachimbaji wadogo?
Kuna haja gani ya kuendelea kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki wakati kampeni zimeisha?