Ni chuma ulete ama ni gharama za maisha zimepanda? Sielewi

Jamani najiuliza ni kwamba nimefungiwa jini chuma ulete ama ni gharama za maisha zimepanda mara dufu?

Yani mpaka sasa hivi nimeshatumia elfu 17 na sijafanya anasa yoyote.

Nimenuna sukari 500
Maandazi 2000
Majani ya chai 100
Mkaa 1200.

Watoto hawajala mayai miezi sita na mmoja ni mgonjwa wakanunua mayai manne wagawane 1600, na maziwa ya unga ya lacto kwa mgonjwa kipaketi ni 500.

Watoto wanalalamika siku nyingi wanakula majani kama mbuzi na Dona. Leo waliomba sana nyama. Kwa sababu familia ni kubwa nimeshindwa nusu kilo haitawatosha basi nimeshindwa. Wanaomba tupike chapati nikanunua unga wa ngano kilo na nusu 3000 na mafuta ya kupika ya 2000.

Kwa kweli tutakanda unga na tumafuta kiduchu halafu tupike chapati kavu kama parata.

Nikashauri huku nikiwa na aibu kuu, maana napambana haswa kila siku na hustle kuliko diamond lakini hela inaishia magengeni, hospital, sokoni, nauli.

Nikiwa na aibu hivyo mwanangu akaniambia basi tukanunue nyanya za mia tatu, karoti za mia tatu, bamia za mia mbili, hoho mia mbili, na vitunguu mia mbili. Nimepewa nyanya tatu, bamia nne, vitunguu viwili, karoti tatu tupike mchuzi wale na hizo chapati.

Yani nimepambana na hustle kinyama lakini nateseka na hii familia ya watoto wanne na wazazi wawili. Halafu kweli maisha hayana haki wengine wana mahelaa. Na ujue mimi sikua maskini nilikua na maisha yangu lakini kiongozi mmoja akaamua kuniumiza kwa kuchukua haki yangu na kwa kuwa sina nguvu basi na mamlaka wala sina connection ndo hivyo nikawa na hali hii.

Pamoja na yote sitauza mwili wangu, naumia sana napoona mwonevu anatamba na wanapewa nafasi za uongozi wakati mimi nateseka na familia yangu.

Nimeanza kuwachukia wanasiasa sana. Waonevu na hawana haki wanatetea makabaila wenzao.

Kilichoniuma sana mtoto amedondosha shilingi elfu moja yani tumeitafuta mpaka tumerudi dukani lakini hatujaipata.

Mimi natafuta elfu huku watu wana millions. 2000 nimelipa deni la majani ngogwe bamia na Dona.

Mniombee niweze kumudu gharama za uendeshaji wa hii familia. Kuna saa natamani hata nijichome moto navyo feel guilty mbele ya hawa watoto. Kuna saa wanauliza mzazi wetu mbona sasa huyu aliekunyang’anya mali analindwa hivyo na serikali?

Unakumbuka tulikuwa hatulali njaa? Hatutembei umbali mrefu kwenda kanisani ama shule?

Anyways, nitafanya yote lakini sitajiuza.

Nina hasira sana, napika saa hizi ili usiku tusipike. Ndo kawaida yangu mlo mara mbili ama moja

Tatizo mlipokuwa nazo mlikuwa show offs na kudharau wengine nyodo na majivuno. Maneno ya watu huumba.
 
Tatizo mlipokuwa nazo mlikuwa show offs na kudharau wengine nyodo na majivuno. Maneno ya watu huumba
Tatizo mlipokuwa nazo mlikuwa show offs na kudharau wengine nyodo na majivuno. Maneno ya watu huumba.

Tatizo mlipokuwa nazo mlikuwa show offs na kudharau wengine nyodo na majivuno. Maneno ya watu huumba.
Ulikuwepo.master? Well tuseme nilikuwa na show offs, je gharama za maisha huko kwako hazijapanda? Watu wanaokuzunguka wanakula Milo mingapi? Wananchi wakienda ofisi za serikali wanatatuliwa kero zao kwa haki na kwa wakati? Je wenye nazo hawana showoffs?
 
Never give up, everything gonna be alright, Work Hard, Pray Hard

Jamani najiuliza ni kwamba nimefungiwa jini chuma ulete ama ni gharama za maisha zimepanda mara dufu?

Yani mpaka sasa hivi nimeshatumia elfu 17 na sijafanya anasa yoyote.

Nimenuna sukari 500
Maandazi 2000
Majani ya chai 100
Mkaa 1200.

Watoto hawajala mayai miezi sita na mmoja ni mgonjwa wakanunua mayai manne wagawane 1600, na maziwa ya unga ya lacto kwa mgonjwa kipaketi ni 500.

Watoto wanalalamika siku nyingi wanakula majani kama mbuzi na Dona. Leo waliomba sana nyama. Kwa sababu familia ni kubwa nimeshindwa nusu kilo haitawatosha basi nimeshindwa. Wanaomba tupike chapati nikanunua unga wa ngano kilo na nusu 3000 na mafuta ya kupika ya 2000.

Kwa kweli tutakanda unga na tumafuta kiduchu halafu tupike chapati kavu kama parata.

Nikashauri huku nikiwa na aibu kuu, maana napambana haswa kila siku na hustle kuliko diamond lakini hela inaishia magengeni, hospital, sokoni, nauli.

Nikiwa na aibu hivyo mwanangu akaniambia basi tukanunue nyanya za mia tatu, karoti za mia tatu, bamia za mia mbili, hoho mia mbili, na vitunguu mia mbili. Nimepewa nyanya tatu, bamia nne, vitunguu viwili, karoti tatu tupike mchuzi wale na hizo chapati.

Yani nimepambana na hustle kinyama lakini nateseka na hii familia ya watoto wanne na wazazi wawili. Halafu kweli maisha hayana haki wengine wana mahelaa. Na ujue mimi sikua maskini nilikua na maisha yangu lakini kiongozi mmoja akaamua kuniumiza kwa kuchukua haki yangu na kwa kuwa sina nguvu basi na mamlaka wala sina connection ndo hivyo nikawa na hali hii.

Pamoja na yote sitauza mwili wangu, naumia sana napoona mwonevu anatamba na wanapewa nafasi za uongozi wakati mimi nateseka na familia yangu.

Nimeanza kuwachukia wanasiasa sana. Waonevu na hawana haki wanatetea makabaila wenzao.

Kilichoniuma sana mtoto amedondosha shilingi elfu moja yani tumeitafuta mpaka tumerudi dukani lakini hatujaipata.

Mimi natafuta elfu huku watu wana millions. 2000 nimelipa deni la majani ngogwe bamia na Dona.

Mniombee niweze kumudu gharama za uendeshaji wa hii familia. Kuna saa natamani hata nijichome moto navyo feel guilty mbele ya hawa watoto. Kuna saa wanauliza mzazi wetu mbona sasa huyu aliekunyang’anya mali analindwa hivyo na serikali?

Unakumbuka tulikuwa hatulali njaa? Hatutembei umbali mrefu kwenda kanisani ama shule?

Anyways, nitafanya yote lakini sitajiuza.

Nina hasira sana, napika saa hizi ili usiku tusipike. Ndo kawaida yangu mlo mara mbili ama moja

Ukisoma makundi ya chakula vizuri familia haitadhurika na diet
 
unapopata changamoto za kimaisha anza na wewe mwenyewe kujifikiria ulikosea wapi na wapi ulifanya sahihi, sio kila tatizo lako limesababishwa na watawala.
 
Pole sana mkuu.... mzazi mwenzio hayupo walau kupeana kampan kutunza family ?

Fikiria namna bora ya kukuza kipato chako kwa sasa, ukifikiria kazi ulioipoteza kwa dhulma utazidi kuumia kifikra
 
Kama umeweza kufanya hayo AMINI unaweza kufanya zaidi..... never say never
 
Ungekua unaendelea kula keki ya taifa ungekuja kutuambia kua kuna nafuu unaipata huko,
Mungu huwafungulia ila mnajisahau,pengine kuna mtu alishakulalamikia na wewe mahala
Ukipanda kumbuka iko siku utashuka,na usiposhuka utashuka kwa kufukiwa,tuishi kwa nidhamu na kila mtu
 
Kweli maisha yanatofautiana.
Hapa mimi nina mahindi ya kula ugali na familia yangu ya watu watano mpaka mwakani mwezi wa nne..
 
Mpige tafu huyo member apate kushibisha wanae pia, Mungu atakuzidishia
 
Asikwambie mtu siasa za Tanzania hasa za ccm zinaumiza mno kuliko mapenzi au kufiwa na ndugu.
 
Ungekua unaendelea kula keki ya taifa ungekuja kutuambia kua kuna nafuu unaipata huko,
Mungu huwafungulia ila mnajisahau,pengine kuna mtu alishakulalamikia na wewe mahala
Ukipanda kumbuka iko siku utashuka,na usiposhuka utashuka kwa kufukiwa,tuishi kwa nidhamu na kila mtu
Nani alikuambia mi nimewahi kula keki ya Taifa, wewe ndo una Dola laki tatu ndani? Huwezi ona gharama ya maisha huku mitaani
 
Back
Top Bottom