Jamani najiuliza ni kwamba nimefungiwa jini chuma ulete ama ni gharama za maisha zimepanda mara dufu?
Yani mpaka sasa hivi nimeshatumia elfu 17 na sijafanya anasa yoyote.
Nimenuna sukari 500
Maandazi 2000
Majani ya chai 100
Mkaa 1200.
Watoto hawajala mayai miezi sita na mmoja ni mgonjwa wakanunua mayai manne wagawane 1600, na maziwa ya unga ya lacto kwa mgonjwa kipaketi ni 500.
Watoto wanalalamika siku nyingi wanakula majani kama mbuzi na Dona. Leo waliomba sana nyama. Kwa sababu familia ni kubwa nimeshindwa nusu kilo haitawatosha basi nimeshindwa. Wanaomba tupike chapati nikanunua unga wa ngano kilo na nusu 3000 na mafuta ya kupika ya 2000.
Kwa kweli tutakanda unga na tumafuta kiduchu halafu tupike chapati kavu kama parata.
Nikashauri huku nikiwa na aibu kuu, maana napambana haswa kila siku na hustle kuliko diamond lakini hela inaishia magengeni, hospital, sokoni, nauli.
Nikiwa na aibu hivyo mwanangu akaniambia basi tukanunue nyanya za mia tatu, karoti za mia tatu, bamia za mia mbili, hoho mia mbili, na vitunguu mia mbili. Nimepewa nyanya tatu, bamia nne, vitunguu viwili, karoti tatu tupike mchuzi wale na hizo chapati.
Yani nimepambana na hustle kinyama lakini nateseka na hii familia ya watoto wanne na wazazi wawili. Halafu kweli maisha hayana haki wengine wana mahelaa. Na ujue mimi sikua maskini nilikua na maisha yangu lakini kiongozi mmoja akaamua kuniumiza kwa kuchukua haki yangu na kwa kuwa sina nguvu basi na mamlaka wala sina connection ndo hivyo nikawa na hali hii.
Pamoja na yote sitauza mwili wangu, naumia sana napoona mwonevu anatamba na wanapewa nafasi za uongozi wakati mimi nateseka na familia yangu.
Nimeanza kuwachukia wanasiasa sana. Waonevu na hawana haki wanatetea makabaila wenzao.
Kilichoniuma sana mtoto amedondosha shilingi elfu moja yani tumeitafuta mpaka tumerudi dukani lakini hatujaipata.
Mimi natafuta elfu huku watu wana millions. 2000 nimelipa deni la majani ngogwe bamia na Dona.
Mniombee niweze kumudu gharama za uendeshaji wa hii familia. Kuna saa natamani hata nijichome moto navyo feel guilty mbele ya hawa watoto. Kuna saa wanauliza mzazi wetu mbona sasa huyu aliekunyang’anya mali analindwa hivyo na serikali?
Unakumbuka tulikuwa hatulali njaa? Hatutembei umbali mrefu kwenda kanisani ama shule?
Anyways, nitafanya yote lakini sitajiuza.
Nina hasira sana, napika saa hizi ili usiku tusipike. Ndo kawaida yangu mlo mara mbili ama moja