mojax
Member
- Aug 18, 2015
- 13
- 23
ELIMU BIASHARA
NI CHANGAMOTO TU, USIHISI TULIANDALIWA KUFELI?
Inawezekana katika maisha yetu tuliyokulia tangu tukiwa watoto tumekuzwa katika Maisha ya kuogopa au kuogopeshwa. Kila ukifanya kitu cha kitofauti unakanywa na kuambiwa ubaya wake badala ya uzuri wake, hata wakati unajenga vyungu vya Udongo kinyumbani ulikatazwa ukiambiwa wachafuka na kuchafua Nguo, ila uliruhusiwa kama ilikua ni Project ya Shule. Lakini mara chache tumekua tukifundishwa hivi shule, Je tuilaumu Elimu? Au tulaumu wale ambao hawakutupa chance ya kuvijaribu tukiwa Nyumbani?
Kwa mfano, Chukua watoto waweke kwenye Makundi mawili, Kundi moja wawe wenye Akili sana, na kundi jingine wale wasio na Akili (Vilaza) , zen wape mtihani wa fumbo sawa. Ni wazi wenye akili watafaulu, hawa vilaza watafeli. Zen wachukue wale vilaza na anza kuwafundisha kwa maswali mepesi, wakielewa wape maswali magumu kidogo na wafundishe jinsi ya kuyatatua na nin cha kufanya kama swali ni gumu. Ukiona wamefikia level ya uelewa kama wale Vichwa wengine waweke tena darasa moja na wale wenye akili, wape mtihani wa fumbo utakaokua Mgumu kwa wote, unajua nini kitatokea?
Wale Vilaza watafaulu zaidi ya hawa Vichwa, kwasababu wamefundishwa kwa hatua jinsi ya kukabiliana na magumu na jinsi ya kuyatatua, hawa vichwa wamezoea tumia akili zao kwakua wanajiamini na hili ni Gumu watafeli, na kupitwa na vilaza kutawafanya waghafirike. Maisha ya shule yalitakiwa yatufunze Jinsi ya kuja kukabiliana na changamoto za Mtaani, Maisha ya shule hayakutakiwa kutufundisha ufaulu ili tuje kupata kazi nzuri. Maisha ya Nyumbani yalitakiwa yatujenge katika Sapoti, ukomavu wa akili na moyo wa kujaribu mpaka kufanikiwa, sio moyo wa woga kwa kuogopa tutakuja kufeli. Mlee mwanao aje kuzikabili Changamoto za kwenye Maisha yake, Kiakili na Kimalezi.
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
By Man Dea
Instagram Follow: Elimu_biashara

Last edited by a moderator: