Ni bora ushikwe na kichaa au malaria kuliko ushikwe na mke wa mtu

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Nyie acheni tu. Ni bora ushikwe na kichaa kuliko kushikwa na mke wa mtu; Ni bora ushikwe na Malaria kuliko kushikwa na mke wa mtu.

Ilikuwa Jumapili, mwanenu, siku hiyo nimeamka mapema mithili ya maiti iliyofufuliwa.

Nikaingia bafuni kuyapiga maji kama vile yalinikosea sasa nalipa kisasi na yatanikoma. Baada ya kama dakika kumi hivi nikachomoka bafuni fasta nikazama tena Ghetto kuvaa ili niende kijiweni kutulia. Basi kidogo tu nikavaa chapu na kabla ya kuibuka kijiweni nikaamua nipite cafe: sio ile ya intaneti, nazungumzia ile ya misosi ili nidake kifungua kinywa mithili ya Juma Kaseja wa mechi ya Kenya na Bongo halafu baadae nisukume na toothpick ya bure bila hata ya kula nyama.

Kati kati ya msosi, Si akatokea Chick f'lani - Main sio main yaani side sio side. Amekula high waist jeans na kitop hivi akawa kama ana display muonekano wa nyuki kwa kutumia mwili wa binadamu "Ass Fat, And thick waist". Akaja akaketi kwenye meza niliyokaa zikaanza stori na utani, Vicheko na uongo hadi kidogo dogo nikacheza blunder ya kubadilishana namba na akaahidi kulipa bill mimi hata nisijali. Nikawaza how comes nime order a cheap meal halafu inakuja ofa ya kulipiwa. Lakini ndiyo hivyo, "Ng'ombe wa maskini hazai".

Basi tukaachana. Yeye akadandia kwenye IST yake ilivyokuwa nje na mimi nikala kona kivyangu - Kuna wakati natamani ni bora ningekula hata penalty aisee.

Mguu mosi, Mguu pili hadi kijiweni. Stori mbili tatu na wana zikaanza. Uongo na chai za kupotezea muda mara maajabu ya dunia yakatokea, Simu yangu ikaita na ni nadra sana mimi kupigiwa simu. Aisee, Ningejua nisingepokea ila ndiyo hivyo, kiherere hakijawahi acha mtu salama.

Nikapokea mara nikasikia, "Hello, baby". Sikumbuki ilikuwaje ila nachojua kilichofuata mimi nipo nyumbani kwa yule Chick sebuleni.

Nikasaviwa Sharubati baridii. Mzee nikaanza kuipiga pole pole kama vile sitaki iumie... Wazee, kukosea sio mpaka unywe bia tu. Nilikula home made juice na nikalewa! Kichwa cha juu kikaachia kazi ya kufikiria ibakie kuwa ya kichwa cha chini.

Kilichofuata ni tumelala hoi kwa sababu ya uchovu. Mara mlango ukagongwa, kumbe ni bwana yake na demu amerudi bila ya taarifa! Sababu ya uchovu nikashindwa hata kufikiria namna nzuri ya kujificha basi nikajichimbia tu kwa shuka nikae kama mto.

Si demu akamfungulia jamaa akapenya, Mara akaja moja kwa moja kitandani akani poke. Ikawa ni kama karuhusu mto umwage maji - Nikajikuta nakojoa bila kuelewa. Nikawa mto kweli kweli!!

Kati kati ya kukojoa nikaanza kusali, lakini amini usiamini, kuna wakati hata ukisali bado hausalimiki. Sijui ilikuwaje nachojua ni kuwa suruali nilienda kuvalia kati ya migomba na ndala nilinunua kesho yake. Yaani miguu ndiyo iliniokoa!!
 
Unatumia jina ambalo pia ndo jina langu , ungetumia hata nickname
 
Back
Top Bottom