Ni baki na yupi?

Ni baki na yupi?

Confundido

Member
Joined
Mar 17, 2021
Posts
56
Reaction score
162
Kwema wakuu

Kwa wiki kadhaa sasa nimejikuta nikikosa usingizi kutokana na mawazo. Ni hivi:

Nilitengana na mama wa mtoto wangu mwanzoni mwa mwaka 2021. Aliniachia binti yetu wa kike ambaye nimekuwa nikimlea peke yangu. Kwa sasa ana umri wa miaka 7. Tangu hapo nimekuwa nikitegemea msaada wa majirani kwa mambo mbalimbali ya kulea mtoto.

Mwaka jana, takribani mwezi wa saba, nilipata mpenzi mpya. Hatukuwa tunaishi pamoja rasmi—huwa anakuja kwangu na kuondoka. Wakati mwingine anaweza kukaa kwangu hata wiki nzima, lakini pia kuna nyakati tulitengana hadi kufikia miezi mitatu. Mwaka huu kuanzia mwezi wa tatu, alianza kutulia kidogo kwangu.

Tulijaribu mara kadhaa kupata ujauzito lakini hatukufanikiwa. Nilimweleza wazi nia yangu ya kutaka kumuoa, lakini alikuwa ananiambia hayuko tayari kwa sasa. Wakati huo, nilikuwa nimechoka sana kuishi maisha ya upweke bila mke. Nilijaribu hata kutafuta mwenza kupitia mitandao, lakini haikufanikiwa.

Mpaka siku moja nikampigia simu mama mtoto wangu na nikamueleza nia yangu: kwamba turudiane, tulee mtoto wetu pamoja na tuongeze familia. Alikubali, akaja, tukasameheana na maisha yaliendelea vizuri.

Lakini kabla hata mwezi haujaisha tangu turudiane na mama mtoto, mpenzi wangu wa zamani alianza kunisumbua akisema ni mjamzito. Baada ya vipimo, ikathibitika kweli ni mjamzito.

Kinachonipa mawazo sasa ni hivi:
Mpenzi huyo amesema anataka kuutoa ujauzito huo kwa sababu hawezi kumzaa mtoto ambaye hatakuja kuishi na baba yake. Kwa upande mwingine, mimi sina uwezo wa kiuchumi wa kumudu maisha ya wanawake wawili. Hali hii imenichanganya sana, na ndio chanzo cha mawazo yanayoninyima usingizi.

Sijui nifanyaje wakuu nishaurini
 
Nyie ndo wale mnaojinenepea hovyo kiasi Cha kufanana na pipa au jaba maana hakuna mnachowaza.nyie mkila,kunya na kushiba tu ni kuwaza vitu vya kipumbavu tu na hamna mnaloliwaza kuhusu taifa linaloangamia
taifa linajengwa na wengi mkuu siyo Mimi peke yangu, mimi fundi Rangi nasubiria Taifa kwenye finishing
 
Back
Top Bottom