Zee la kitaa
JF-Expert Member
- Oct 25, 2017
- 403
- 211
Kuna wakati ukifuatilia mijadala ya vijana katika mitandao ya kijamii; utaona uwezo wetu wa kufanya uchambuzi wa kutosha ni mdogo katika siasa; uchumi na shughuli za kijamii. Imefikia wakati vijana kutaka kufananisha CCM na chadema bila kutambua mambo matano muhimu:-
- Vyama hivi viwili vinatofauti za itikadi na miongozo ya kiutendaji. CCM ni chama kilicho na itikadi ya wananchi. Ni chama kinachoamini itikadi ya wananchi hususani wa hali ya chini. CCM kuanzia kuanzishwa kwake kilijikita kutetea usawa, maslahi ya wanyonge na siasa za kiustarabu. Chadema ni chama ambacho kimejikita katika itikadi ya wananchi katika misingi ya kiuharakati. Ndio maana Lowasa alipoingia chadema alikuwa anawasihi viongozi wa chadema kuacha uwanaharakati na kujikita na siasa za kisayansi. Kwa msingi huo utagundua chadema na CCM ni vyama vyenye maslahi tofaut;
- Mfumo wa demokrasia. CCM ni chama ambacho kimekomaa katika mfumo wa demokrasia. Ni chama ambacho kinautaratibu unaoeleweka uliowekwa kwa ajili ya kusimamia demokrasia. Ni chama ambacho kimepitia katika vuguvugu za mabadiliko mbalimbali ya kidemokrasia ukilinganisha na chadema. Chadema ni chama chenye mwenyekiti almost tumuite wakudumu ama mkurunzinza. Chadema kinajinasibu kuwa chama cha demokrasia lakini utendaji wake hauendani kabisa. Mgombea urais anotoka huku leo kesho anatangazwa chadema.
- Uimarishaji wa chama. CCM ni chama kilichojiimarisha katika ngazi zote. ni chama ambacho kiko karibu sana na wananchi. kina matawi katika vitongoji na mitaa. Hii itaichukua chadema miaka kadhaa kufikia hivyo.
- Matumizi bora ya rasilimali. CCm ndio chama pekee chenye mustakabali wa kuthamini kutambua rasilimali zake zote na kuimarisha usimamiaji kwa manufaa ya chama. Ruzuku za chama hazina migogoro ukilinganishwa na chadema ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kuwa na mashaka na fedha za ruzuku za chama.
- Kujenga vijana katika uongozi na kusimamia maendeleo ya vijana katika siasa safi. CCM ni chama imara katika kujenga vijana wenye mustakabali wa kushika hitama ya uongozi bora katika taifa hili. CCM hupika viongozi wa badae na hueshimiana katika hilo. CCm inahazina ya viongozi wengi vijana. Chadema ni chama ambacho ingawaje kinatambua kuendeleza vijana lakini kinashindwa kuwasimamia vijana wasimame katika mustakabali wa maendeleo ya rasiliamali ya chama. Wegi wao hukatishwa tamaa na viongozi wao wa juu wanaoteua vijana katika uongozi kwa maslahi yao.