Ni aina gani ya Smart Phone?

GBBS

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
97
Reaction score
48
Wana JF,naomba kujua kutokana na uzoefu wako binafsi aina ya simu ambayo itakuwa ni ya kasi sana na ina uwezo wa kuangalia Youtube,download n.k. bila shida.Pia yenye uwezo ambayo unaweza ukaandika documents mbalimbali na kuziprint moja kwa moja kwenye printer.Yaani kwa ufupi ambayo unaweza ukafanya kazi nyingi bila kuhitajika kutumia Computer.Pia kwa anayejua gharama zake kwa makadirio.Napenda kutumia vitu ambavyo ni "Genuine",hivi fake vina usumbufu sana!.Asante kwa ushirikiano mwema na uwe na siku njema yenye baraka tele za Mungu aliye hai.Nawasilisha.
 
Smartphones nyingi zinaweza kufanya hayo uliyoyataja.
Napendekeza galaxy note 3 kwa sababu ya ukubwa wa screen.
Kuhusu ku-print unaweza uka-download printing app, kama haina.
angalia links hapo chini, zimeelezea kiasi cha kutosha sifa za simu mbalimbali, baada ya hapo unaweza ukaingia you tube ukapata maelezo zaidi kuhusu simu husika.

GSMArena.com - GSM phone reviews, news, opinions, votes, manuals and more...

Phone Arena - Phone News, Reviews and Specs

How to Print From a Smartphone | eHow

Samsung Galaxy Note 3 Review! - YouTube

Samsung Galaxy Note 3 Review - YouTube
 
Chukua samsung S5 ni tshs 2,000,000/- inafanya yote.
 
kaka huwezi print document kutoka kwenye simu ambayo umeitengenezea kwenye simu kwenye printer ya kawaida. printer hizi za mitaani nyingi zipo compatible na microsoft office tu. kama matumizi yako ni hayo hapo tu ina maana wewe unahitaji simu ya windows phone ndio pekee yenye ms office.

kwa vifaa vya apple kama iphone na ipad unaweza create document ila utahitaji printer special hivyo gharama zitaongezeka.

kwa android utaweza create ila ukiprint na printer ya kawaida hakuna uhakika document itatoka kama ilivyo. alignment, paragraph na baadhi ya formating hazitatoka kama zilivyo. ila kama unaprint picha hakuna neno zinatoka vizuri tu.

kuhusu kuangalia youtube na kudownload hizo video karibia smartphone zote za kisasa zinafanya
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ