Ni aibu tupu Uwanja wa Taifa, Serikali angalieni hili

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Nilikuwa Uwanja wa Taifa Leo kuangalia mchezo wa mpira miguu kati ya Simba na Yanga wa Ligi juu Tanzania Bara ambayo imeisha kwa Simba kuifunga Yanga.

Lakini nilichoona Leo mara nilipopata muda wa kuingia ktk vyoo vya uwanja kkwa short call mmmmh ni hatari sana kwa afya za watazaji wa mpira lakini kubwa zaidi ni aibu kwa Taifa.

Jamani jamani kweli maji ni shida au yamefungwa maana kuna madimbwi pia ya maji yasiyoenda sasa sijui vyoo vimeziba...mikojo imejaa haiendi aiseee ni hatari sana.

Serikali ndiyo wamiliki wa uwanja hebu yaangalieni haya mapungufu.

Au uwanja bado unajengwa??
 
Sisi mambo haya kwetu sawa.... huduma hizi za serikali huwa hazina mfuatiliaji mpaka mwisho.... kuna hata taasisi za serikali kama mwanza city choo zao ni shida....
 
Mhh! Huu uchochezi
Ni aibu sana bwana haifai kabisa kuonana hali kama hiyo na tunaendelea na maisha tu.

Vyoo vingine vimejaa kinyesi ni aibu sana na kumbuka mass ya watu inayokwenda pale

Na Kigamboni Municipal kuna wagonjwa wa kipindupindu kwa taarifa ya Serikali na mmoja alifariki juzi tu.

Kinga ni bora kuliko tiba
 
Sidhani km kuna shabiki wa simba ana mda wa kuliona hilo kwa kazi walioifanya leo wewe lazma utakuwa shabiki mwenzangu wa mateja fc ukaona niangalie cha kutoka nacho baada ya kushindwa kutoka na hata na droo dhidi ya watu pungufu
 
Mateja FC hahaaaa
 
Sisi mambo haya kwetu sawa.... huduma hizi za serikali huwa hazina mfuatiliaji mpaka mwisho.... kuna hata taasisi za serikali kama mwanza city choo zao ni shida....

Ni obvious kuna Mawaziri husika wanapita humu, kuna mwenzao alienda kufagia na kudeki wodi ya wagonjwa Muhimbili kama sijakosea haya sasa nao waoneshe mfano kama kweli wapo kikazi zaidi
 
Ni aibu sana bwana haifai kabisa kuonana hali kama hiyo na tunaendelea na maisha tu.

Vyoo vingine vimejaa kinyesi ni aibu sana na kumbuka mass ya watu inayokwenda pale

Na Kigamboni Municipal kuna wagonjwa wa kipindupindu kwa taarifa ya Serikali na mmoja alifariki juzi tu.

Kinga ni bora kuliko tiba

Mkuu tupo pamoja sana tu. Ila nchi yetu timefika pabaya sana kuwa kila ukweli dhidi ya wahusika ni uchochezi. Sijui nchi hii tunaelekea wapi!!!.
 
Nilikuwa Uwanja wa Taifa Leo kuangalia mchezo wa mpira miguu kati ya Simba na Yanga wa Ligi juu Tanzania Bara ambayo imeisha kwa Simba kuifunga Yanga.

Lakini nilichoona Leo mara nilipopata muda wa kuingia ktk vyoo vya uwanja kkwa short call mmmmh ni hatari sana kwa afya za watazaji wa mpira lakini kubwa zaidi ni aibu kwa Taifa.

Jamani jamani kweli maji ni shida au yamefungwa maana kuna madimbi pia ya maji yasiyoenda sasa sijui vyoo vimeziba...mikojo imejaa haiendi aiseee ni hatari sana.

Serikali ndiyo wamiliki wa uwanja hebu yaangalieni haya mapungufu.

Au uwanja bado unajengwa??
Tatizo ni kwamba watumiaji hatuna uungwana. Usafi na ustaarabu kwenye sehemu za kujistiri za umma sio desturi zetu wabantu.
 
Tatizo halipo kwa serikali
tatizo ni Mijitu isiyo jitambua
uchafu wa asili
hii ni hatari
lakini kama serikali ikiadhibu watu hao
ninyi wenyewe ndio wakwanza kuingiza siasa na kupinga!!
 
Tafta number ya simu ya makonda umueleze mapema kabla jumatatu haijafika siku yake ya kutumbuliwa
 
Vile vyoo vya taifa kwa kweli ni aibu!
Niliwahi ingia pale ikabidi niahirishe haja...
 
Vile vyoo vya taifa kwa kweli ni aibu!
Niliwahi ingia pale ikabidi niahirishe haja...
Mimi sijui tatizo liko wapi kuhusu vyoo vya Uwanja wetu wa Taifa ambao hata Drogba alipokuja alisema ni moja ya viwanja bora kabisa Africa.

Tunamshukuru Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa kujenga uwanja huu lakini tunashindwa kuutunza kweli ni aibu sana.
 
Back
Top Bottom