Ni Aibu kwa Wabunge wa Upinzani Kuuliza Maswali kupitia Wabunge wa CCM

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Haya ni maoni yangu tu,

Ni mara mbili nimesikia wabunge wa upinzani wakiwatumia wabunge wa CCM kuuliza maswali katika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni.

Mara ya kwanza: Niliona Chatherine Magige (MB) Viti Maalum Arusha CCM akiuliza swali kwa niaba ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Sugu kuhusu Ujenzi na Hospitali ya Kanda ya Mbeya. Alipouliza swali la nyongeza akasema kwa vile Hospitali Mauti Meru ni Muhimu zaidi ya Kanda ya Mbeya na hatuna hata vifaa vya kuchunguza magonjwa, unasemaje juu ya hili.

Mara ya Pili: Mbunge wa Busega Dk. Raphael Chegeni kuuliza sababu za Halmashauri na miji inayongozwa na Upinzani kutumia Ila ya CCM katika kazi zake. Swali la nyongeza Chegeni akauliza namna gani bunge litawabana wanaotoka katika mijadala ya Bunge.

Imenifanya nifikiri azma ya kuuliza maswali kwa kutumia wapinzani wao kutoka CCM. Hawa kila siku tunasema hawafai na hawana uelewa. Imekuweje wasimamie hoja za kipinzani bungeni?

Hii itakuwa na tija? Kama unapata nafasi ya kuuliza swali la Msingi najua unatakiwa uulize ma/swali la nyongeza na ndo yanakuwa na ufafanuzi zaidi ya lile swali la kwanza.

The Gaza
 
Taarifa na malengo yao hayafikishwi kama yalivyo. Pia hakuna wa kulinda mawazo yao.

Mkubwa hapo wanakuwa walau wamepewa fursa ya kusikika wakisema mambo ya msingi japo linapokuja swali la nyongeza wanajikuta wamerudi kwenye asili yao ya kuomba viwanja vya kumbukumbu ya push-ups na masanamu ya Diamond.
 
Lazima ifike wakati wakubaliane na hali ya bunge ili watetee waliowachagua kwani kama ni UJUMBE umefika, hivi kweli wanadhani kwa siasa zetu upande wa pili unaweza kuunga upande mwingine kwa masilahi yake? Wabunge hapo watumie BUSARA ili HADHI ya bunge iendelee kuwepo. Watakaa nje na maamuzi ya kuwaonea yatatekelezwa kirahisi pengine wangekuwepo AIBU ya ubinadamu ingesaidia. Tanzania tulipofika lazima pande zote za kisiasa kuvumiliana kutokana na kuwa na tabia,makuzi,hulka,mazoea,falsafa tofauti kutokana historia ya vyama vyetu hivyo wakubali warudi ndani ya bunge kwa nia ya kuruhusu kusikia mawazo yao mbadala ambayo jamii imeyakosa pia mbona wamekuwa wakikubali kushiriki chaguzi ilihali wakiwa hawana imani na tume? IMETISHA UJUMBE UMEFIKA
 
Kwani wamekatazwa kurudi bungeni? wakirudi bungeni wanakufa? waache waendelee kukaa nje kwa maslahi ya Chama
 
Hivi huyu mbunge wa ukonga anaongelea wapi matatizo yetu? Mbona sioni hata kinachoendelea?
 
Kama hujui taratibu za kibunge kaa kimya.
Hao wabunge wako wa CCM tunawaandikia maswali ya kuuliza kwakua wao hawako hapo kuhoji bali kusema ndiyooo.
 
Kanuni inaruhusu ya 42(1) inasema iwapo mbunge anayetakiwa kuuliza swali hata kuwepo basi Spika atamuita mbunge yeyote kuuliza swali husika. Kwahiyo huo ni uamuzi wa Spika mwenyewe ili maswali yapate kuulizwa kama yalivyopangwa katika orodha ya shughuli kwa siku husika
 
Nafikiri kwa kuwa wabunge wa UKAWA hutoka nje ya ukumbi wa bunge vikao vinapoendeshwa na naibu wa spika, na kwa kuwa maswali yaliyoulizwa na wabunge wa upinzani yanakuwa yamepangwa kuulizwa siku husika, naibu spika humteua mbunge wa CCM aulize kwa niaba ya mbunge wa upinzani aliyeuliza swali ili shughuli za bunge zisikwame. Hivi ndivyo ninavyofikiri, sina hakika kama ndivyo.
 
Shida iko wapi...km wote ni wabunge wa wananchi.

Wewe huoni mgongano kwenye swali la Sugu kuhusu hospital ya Kanda.?
Ametumwa akaulize swali la msingi, halafu kwenye swali la nyongeza anaponda swali msingi alilotumwa akaulize.!
 
Haya ni maoni yangu tu,

Ni mara mbili nimesikia wabunge wa upinzani wakiwatumia wabunge wa CCM kuuliza maswali katika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni.

Mara ya kwanza: Niliona Chatherine Magige (MB) Viti Maalum Arusha CCM akiuliza swali kwa niaba ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Sugu kuhusu Ujenzi na Hospitali ya Kanda ya Mbeya. Alipouliza swali la nyongeza akasema kwa vile Hospitali Mauti Meru ni Muhimu zaidi ya Kanda ya Mbeya na hatuna hata vifaa vya kuchunguza magonjwa, unasemaje juu ya hili.

Mara ya Pili: Mbunge wa Busega Dk. Raphael Chegeni kuuliza sababu za Halmashauri na miji inayongozwa na Upinzani kutumia Ila ya CCM katika kazi zake. Swali la nyongeza Chegeni akauliza namna gani bunge litawabana wanaotoka katika mijadala ya Bunge.

Imenifanya nifikiri azma ya kuuliza maswali kwa kutumia wapinzani wao kutoka CCM. Hawa kila siku tunasema hawafai na hawana uelewa. Imekuweje wasimamie hoja za kipinzani bungeni?

Hii itakuwa na tija? Kama unapata nafasi ya kuuliza swali la Msingi najua unatakiwa uulize ma/swali la nyongeza na ndo yanakuwa na ufafanuzi zaidi ya lile swali la kwanza.

The Gaza
Ccm hawana cha maana cha kuuliza inabidi waulize ya waliyonayo. Pia upinzani bungeni spika anajifanya hawaoni. Huwa anaruhusu yule anayeamua yeye kwa kusema anamuina fulani kasimama. Kupata nafasi ya kuuliza ni maamuzi ya spika.
Tatu bunge limekuwa likifanya kazi za serikali maana ccm hawajui tofauti ya bunge na serikali. Muda wote wanakuwa ama wasemaji wa serikali au watetezi wa serikali
 
Back
Top Bottom