MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,296
Kuchangiana harusi mnaweza tena kwa maelfu na malaki mingi sana ambayo yanachomwa moto kwa siku moja, mbili au tatu tu. Lakini kuchangia kwenye mambo ya maana ya elimu yanayodumu kwenye vichwa vya watu maisha yao yote mnaona tabu!
Amma kwa hakika Tanzania tuna kazi kubwa sana.
Kwanza kuchanga ni suala la utashi.
Pili, binadamu ana sura nyingi (human being, social being, political being, spiritual being, intellectual being, sexual being, nk) na idara zote hizo anawajibika kuzitimiliza kwa namna moja au nyingine. Anapochangia harusi ni mojawapo ya majukumu yake as a social being. Bwana harusi hajamkwapulia cho chote kwa njia ya kodi!
Anapokataa kuchangia maabara pia napo ni wajibu wake kama political being kwa sababu mchangishaji (serikali) ameisha kusanya kodi kutoka kwake na hajampatia taarifa ya mapato na matumizi ili aone kama achangie au la, au achangie wapi.
Kama Kikwete anatumia hiyo psychology ya kwamba kwa vile watu wanachangia harusi basi watachangia maabara, inabidi uprofesa wa kichina amrejeshee jing wang.