Ni aibu kubwa Taifa letu kujifunza Teknolojia kutoka Rwanda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Tunatangaziwa kwa mbwembwe kuwa Taifa letu linaenda kujifunza Teknolojia kutoka Rwanda. So shameful! Taifa ambalo limeshiriki kupigania uhuru wa nchi karibia zote za Afrika. Taifa lenye mamia ya MAPROFESA na wataalamu wa Teknolojia za kila namna.

Kwa hiyo hawa MAPROFESA wetu tunaowalipa mamilioni ya mishahara kwa mwezi, tena waliosomea teknolojia mbalimbali Uchina, Urusi, Marekani, Ujerumani, Uingereza na kwingineko (kwenye vyuo vinavyoheshimika duniani) ni Maprofesa UCHWARA! Tatizo la nchi hii ni kubwa hadi mkuu wetu hajajua tutaanzia wapi. Kwa uwazi kabisa nasema hii ni AIBU KUU!

Mtatiro J
 
Tunatangaziwa kwa mbwembwe kuwa Taifa letu linaenda kujifunza Teknolojia kutoka Rwanda. So shameful! Taifa ambalo limeshiriki kupigania uhuru wa nchi karibia zote za Afrika. Taifa lenye mamia ya MAPROFESA na wataalamu wa Teknolojia za kila namna. Kwa hiyo hawa MAPROFESA wetu tunaowalipa mamilioni ya mishahara kwa mwezi, tena waliosomea teknolojia mbalimbali Uchina, Urusi, Marekani, Ujerumani, Uingereza na kwingineko (kwenye vyuo vinavyoheshimika duniani) ni Maprofesa UCHWARA! Tatizo la nchi hii ni kubwa hadi mkuu wetu hajua tutaanzia wapi. Kwa uwazi kabisa nasema hii ni AIBU KUU!
Mtatiro J
Ule usemi kuwa nabii haheshimiki nyumbani kwao unatutafuna hapa Tanzania na ndilo tatizo kubwa
 
Mmmh Tatizo huwa mnadandia hotuba za mh. Rais na hivyo hamwezi kumwelewa, kwa hiyo akisema wataalam kutoka Rwanda watakuja Tanzania wewe unadharau?

Unafikiri kiwango cha utaalam wa IT cha wataalam wa Rwanda kiko sawa na cha Tanzania?

Rwanda wako hatua mbele dhidi yetu ndo maana hata wanafunzi wa primary wanatumia min computers ilihali kwetu Tanzania mtu anamaliza chuo kikuu hajui hata kuoperate Microsoft Excel.

Pia usemi wa rais ulilenga kuleta ushirikiano wa wataalam wa teknolojia kutoka Rwanda na Tanzania na sio kama unavyolazimisha ili utimize adhima yako.
 
Kwani hatuwezi kujifunza chochote kutoka Rwanda?
Mkuu, hawa CHADEMA ni ndumilakuwili. Kuna watu humu kazi yao kutengeneza nyuzi ili ionekane Rais Hafai. Hawa ndio waliomuangusha Kikwete na sasa wanaelekea kwa Magufuli. Atachemsha
 
kwa uongoz uliopita lazima tujifunze tu. usishangae baba kufundishwa driving na mwanae. kwan wewe mleta mada ulikuwa wap kugombea toka 2005
 
Mmmh Tatizo huwa mnadandia hotuba za mh. Rais na hivyo hamwezi kumwelewa, kwa hiyo akisema wataalam kutoka Rwanda watakuja Tanzania wewe unadharau? Unafikiri kiwango cha utaalam wa IT cha wataalam wa Rwanda kiko sawa na cha Tanzania?
Rwanda wako hatua mbele dhidi yetu ndo maana hata wanafunzi wa primary wanatumia min computers ilihali kwetu Tanzania mtu anamaliza chuo kikuu hajui hata kuoperate Microsoft Excel.
Pia usemi wa rais ulilenga kuleta ushirikiano wa wataalam wa teknolojia kutoka Rwanda na Tanzania na sio kama unavyolazimisha ili utimize adhima yako.
Hivi walimu hatuna wakutufundisha au
 
Back
Top Bottom