Ni 2020: Kwa Bloggers Wote Watanzania

Maybach 255

Member
Jan 25, 2020
18
31
Habari wana jamvi, natumai mko sawa. Ni mwaka mpya na kesho tutakuwa tunaingia February na ningependa kutoa ujumbe mfupi kwa bloggers watanzania, maana mambo yanabadirika kwa kasi, na ni vyema wengi wao waondokane na kukariri.

Toka swala la blogging liwe maarufu nchini, kumeibuka kila aina ya bloggers, wakubwa na wadogo, na baada ya tafiti zangu fupi, makundi haya nimeweza kuyagawa kwenye makundi mawili marahisi: Bloggers wa Kiswahili na Wale wa Kingereza.

Nikianza na wale wa Kiingereza;
Sababu kubwa ya kuanzisha blog za aina hii ni ili kuingiza kipato kwa Google Adsense, na sana sana zina target surfers kutoka SA na Nigeria. Content mara nyingi hutolewa kwenye blog nyingine na kueditiwa kidogo na kuwekwa kwenye blog zao. Njia zianzotumika kupata visits ni kwa ku promote kwenye magroup FB na kununua Paid Traffic.

Sana sana, wamiliki wa hizi blog hawana passion na wanachoandika, wengine Kingereza hawafahamu kabisa. Lengo kuu ni kuingiza pesa. Hata akaunti za Adsense zinanunuliwa, na hawatumii TLD's sana sana, bali subdomains. Haswa Blogger.

Wale wa Kiswahili; Udaku. Mapenzi. Ujasiriamali. Ndizo topic kubwa. Wengi wao wanaandika ilimradi na waaningiza pesa chache mno. Au hawaingizi kabisa. Humu utakuta post za umbea umbea, kuhusu watu maarufu na siasa. Hawana njia maalumu za kuingiza kipato, na baadhi wanajitahidi kuuza Ebooks na Course. Ila process ndefu, na part kubwa inafanyika offline hivyo kufanya waonekane matapeli. Wengi ni matapeli.

Ninamiliki aina zote mbili za tovuti, na ningependa kutoa ujumbe kwa bloggers wenzangu, huu ni mwaka mpya na yale mambo yote ambayo yamekaririwa, yanapaswa yawekewe ubunifu ili matokeo yawe mazuri. Haya ni baadhi ya mambo ambayo ninafanya na yamekuwa yananifanyia kazi vizuri.

1. TLD vs. SubDomains
• Blog nyingi, zinatumia sub domains, hasa kutoka Blogger na WordPress. Hizi zina hasara nyingi kuliko faida, kwa kuwa hupati total creative na technical control. Kwa namna moja au nyingine, itafanya blog yako iwe imature, na kutochukuliwa serious.

USHAURI: Wekezeni kwenye Domain(TLD yoyote inayoendana na ninche yako, .com, .net, .blog, .online). Nyingi zitakuja na SSL Certificate kufanya site ziwe secure. Itakufanya uwe na motisha mpya, dedication na passion.

Consider NameCheap, BlueHost, Google Domains

2. WordPress vs. Blogger (Joomla? )
• Kuendaa na experience yangu, CMS ya WordPress inakupa features nyingi mno za kufanya blog yako iwe interesting. Nyingi kuliko Joomla na Blogger kwa pamoja. Wana themes/templates ambazo ziko Mobile optimizable na zinavutia. Kutokukupa ulazima wa kuwekeza kwenye mambo hayo wakati tovuti yako ni changa. Kingine ni kuwa ni ya bure, utaikuta kwa Webhosting providers na kufanya one-click install. Gutenberg yao inafanya kuandika kuwe fun, na unaweza pata statics zako vizuri tu. Compared to blogger.

• Dashboard iko simple ila sio simple kama ya Blogger. Ila sidhani kama hii ni factor kubwa.

3. Consider Google Webmaster Tools, Analytics na SEO.
• Ili kuwa indexed vizuri google, unapaswa kuwa linked na Webmaster Tools + Analytics. Ukianza kupata sustainable traffic, hii itakusaidia, pale utakapo taka jiunga na Adsense maana data kuhusu traffic watakuwa nazo, na sitemap yako. Hivyo, itakuwa haraka.

• SEO sio lazima, ila ni muhimu kama uko seriou na blog yako na una jali visitor experience na CTR.

4. Kuingiza Pesa.
• Adsense sio njia pekee ya kuingiza kipato kwenye blog yako, zipo nyingi. Ila kwa kuwa hakuna njia rahisi ya kupokea pesa kwa njia ya mtandao. Inakuwa changamoto. Hapa ubunifu ndipo unapoingia.

• Kwanza nikiuliza, mara ya mwisho ulipokuta tangazo kwenye blog ukalibyofa ni lin? Unatakuta haijawahi tokea. Hivyo kwa wale wanaomiliki blog za kiswahili. Kwanza, jitahidi kuwa na blog inayohusiana na mambo yanayoingiliana, au jambo moja specific. Andika mara kwa mara na kuwa specific, hakuna anaependa kuzungushwa wakati kuna sehemu anaweza soma kirahisi.

• Tumia bullet points, na visual elements kuwasilisha ujumbe wako.

• Mbali na Ads, unaweza toa Whatsapp Group Memberships kwa loyal readers. Kutoa Ebooks na Course ambazo kurahisisha process ya malipo, unaweza tafuta Namba ya Malipo(Lipa Kwa) ili kufanya process iwe rahisi na salama kwa nyote.

Process ya kulipa kawaida, inakuwa ndefu na doubtful.

Ahsante.
 
Good analysis..

Nataka nianzishe blog ila nataka nijikite kwenye utalii, sababu ndiyo taaluma yangu hivyo itakua rahisi kuandaa contents.

Lengo kufanya for fun, part-time thing na kuingiza kipato kwa baadae.

Naomba ushauri kwenye hili..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sandet,
• Fanya utafiti... Wasomaj8wako watakuwa wa aina gani, wanapenda nini, na wanategemea kupata nini kutoka kweye blog yako.

• Tafuta jina, utakalotumia.

• Nunua Domain + Hosting.

• Setup Blog yako(fuata tutorial YouTube au lipa mtu aindae)

• Fanya SEO, Fungua Social Media Accounts, Link na Google Analytics + Google Webmaster Tools. (Kupata matokeo mazuri, husisha pro)

• Andika.

• Andika Tena.

• Andika.

• Share kwenye social media na engage na wasomaji wako.

• Download WordPress app kwenye simu yako ili kuandika wakati wowote.

• Monetise ukihisi ni wakati sahihi.

Goodluck. (Inahitaji uvumilivu, muda kutimiza milestone zako)
 
Wordpress ni kwa wale wenye uzoefu but kwa beginners haiwafai hiyo....for me Nina uzoefu wa kutosha tu lakini situmii WordPress natumia blogger na napiga hela Safi tu
 
Blogu? Tz? Are u serious? If Ur not please be just for a second.

Blogs zishakufa toka Enzi za Pontyo wa Pilato
 
Hali ni tete kwasasa.

Google wanabana huku Facebook wanabana huku, daaaah
 
NAONGEZEA :

Ujikua seo vizuri unaweza kuvamia nchi yoyote ukamake mpunga wakutosha .

Tafuta niche yako, fanya keyword analysis tumia tools kama google trends , tengeneza unique content za kutosha.. usisahau kukonect site yako na google analyts + google webmaster tools.

Tumia google webmaster tools kumonitor keywords ranking fanya improvemnt ya content yako.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Blogu? Tz? Are u serious? If Ur not please be just for a second.

Blogs zishakufa toka Enzi za Pontyo wa Pilato
Ni sahihi kabisa kwa mawazo yako coz c kila mtu anatakiwa amiliki blog.
Ungekuwa unajua kuwa hujui chochote kuhusu digital platforms ungetulia uelimishwe..
Tangu nilivyograduate university (computer eng) sijawahi kuomb kazi mwaka wa 5 sasa coz digital platforms inanifanya nijitosheleze tu...
Watanzania wengi wanapig pesa ila ni wachoyo kushare kwa wengine included me coz wabongo wengi hawapend kujifunza wanapenda vitu vya chap ukimwambia unaweza ukasota ata mwaka mzima ukiwa bado unatengeneza brand anaona kama unamchelewesha maisha.
Ndio maana wengi wanakurupuk mara Blog, youtube channel, Forex, Crypto biz.
But zote hizo zina pesa ila ukitulia na kuamua kujifunza, tukumbuke kuwa hizo ni biashara kam biashara zingine u must pay money, time and brain to learn .
NO EASY MONEY IN THIS WORLD..!!!!
 
Watu wanakimbi Affiliate online alafu wanaenda kariakoo kuchukua viatu, nguo na simu na kuanza kutafuta wateja ili wauze waishi kwa commission.
Sasa sijajua wanakwepa nini wakati wanajiongezea tu mzigo coz mpaka unishawishi ninunue godoro, nguo nk lazim utulie.
We are supposed to change our altitude and mind.
 
Watu wanakimbi Affiliate online alafu wanaenda kariakoo kuchukua viatu, nguo na simu na kuanza kutafuta wateja ili wauze waishi kwa commission.
Sasa sijajua wanakwepa nini wakati wanajiongezea tu mzigo coz mpaka unishawishi ninunue godoro, nguo nk lazim utulie.
We are supposed to change our altitude and mind.
Very True!
 
Back
Top Bottom