Nhunga unaipeleka wapi yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nhunga unaipeleka wapi yanga

Discussion in 'Sports' started by domo bwakubwaku, Mar 3, 2011.

 1. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mambo yanavyoendelea Yanga ni kama maigizo vile juzi kamati ya utendaji imeridhia kuondoka kwa alie kuwa mfadhili wa yanga Bw. Manji katika hali ya kushangaza jana kaibuka mwenyekiti wa Yanga Bw. Loyd na kumwangukia manji arudi yanga, hivi hawa viongozi waliopo yanga walisukumwa na nini kwenda pale yanga au ni kwa ajili ya ulaji? na kazi yao wao pale ni nini? matarajio yangu ni kuwa kuondoka kwa MANJI Yanga ingekuwa ndio chachu ya mafanikio kwa viongozi wake kuja na mbinu na mawazo chanya ambayo yangeifanya Yanga ijitegemee kwa kutumia rasilimali watu na rasilimali nyingine zilizopo kiongozi wa aina ya Nchunga ni tatizo sio kwa Yanga tu bali kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya soka la bongo kwa ujumla KAMA YANGA ITAPATA VIONGOZI WASIO NA FIKRA MGANDO YANGA NI TAJIRI ZAIDI YA MANJI wana YANGA amkeni sasa mbona kama vile ni kurudi nyuma hatua ishirini zama za kina MANJI zilishapita tangu zamani
   
Loading...