NHIF wekeni uwiano wa matibabu kwa watumishi na watu binafsi

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
859
Habarini,

NHIF wekeni uwiano wa matibabu kwa watumishi na watu binafsi wote wachangie sawa na wapate huduma sawa.

NHIF mnapotoa vifurushi vya TUNAJALI,TIMIZA,n.k na kuondoa malipo ya vipino kama vile OGD na kadharika wananchi tunashindwa kuwaelewa kabisa.

Mtu analipia kifurushi cha TIMIZA anasafiri kuja kwenye matibabu MNH Dar Es Salaam anafika anaambiwa apime vipimo ikiwemo OGD halafu anaambiwa alipie kwani haviko kwenye vifurushi vya binafsi sasa kipimo cha OGD tu ni Tshs. 260,000/= ukiacha vinginevyo ambavyo haviko kwenye kifurushi cha TIMIZA.

Kifurushi cha TIMIZA ni Tshs. 1,188,000/= kwa mwaka na mtumishi wa chini analipa Tshs.18,000/= kwa mwezi ukizidisha kwa mwaka/miezi 12 ni Tshs. 216,000/= kwa mwaka.

Sasa mtumishi wa serikali analipia Tshs. 216,000/= kwa mwaka na anapata vipimo vyote na wategemezi 6 iweje mtu binafsi anayelipia Tshs. 1,188,000/= kwa mme na mke tu kwa mwaka asipate vipimo vyote?

Huu ni unyonyaji kwani ni wazi watu binafsi wanaumizwa zaidi na kuwa wabebaji wa gharama za watumishi wa serikali.

Ni wazo langu kuwa kuwe na kifurushi sawa kwa watumishi wa umma na watu binafsi kwa kuchangia gharama sawa na kupata huduma sawa,kama ni kulipia hiyo 1,188,000/= kwa mwaka basi wote walipie kiasi hicho eidha kwa awamu au kwa mkupuo.

Nawasilisha
 
Daaah!!
Sikuwahi kujua uhuni huu!!!
Huu ni uhuni, ushenzi, upumbavu na ufirauni kabisa!
Ndio maana wasiokuwa watumishi wa umma wanapata tabu sana kwenye gharama za afya
 
Natamani hii serikali itoe fursa ya kutibiwa kwa watanzania wote.

Hizo hela wanazotuibia kwenye vifurushi , makato benki etc ni bora zaidi zingelipia bima ya afya kwa watanzania wote.

Ukitaka kujua umuhimu wa bima ya afya ni pale unapokuwa na mgonjwa ambaye inabidi mmchangie gharama za matibabu na dawa kila siku.
 
Back
Top Bottom