Hili ndilo suluhisho la kudumu. Mtu akiajiriwa tu kabla hajapata hata kadi ya Bima wao tayari wanakata Chao.
Ilitakiwa iwe hiari hapo mashirika/mifuko binafsi itaimarika na kuweka ushindani kuliko hali iliyopo sasa. NHIF na kila siku Wanaweka masharti ili watu wasiweze kuweka wanufaika katika Bima zao na wanatoa baadhi ya huduma kwa mnufaika wa Bima.
Wakugoogle unayasema hayo labda kwa sababu hujawahi kupata shida kubwa ya matibabu katika familia yako.
Nataka nikuhakikishie kwamba katika utaratibu wa Bima ya Afya ndani ya AFRICA.......NHIF-TANZANIA inaweza kuwa the best compared na mifumo ya Bima iliyopo Nchi nyingine zote.
Mtumishi wa umma ambaye ni mwanachama wa NHIF ana uhakika wa kupata urahisi wa matibabu kama ifuatavyo:-
1. kwanza anatibiwa yeye mwenza wake na wategemezi 4.
2. Mtumishi anaruhusiwa kuwabeba wazazi na wakwe kama wategemezi .....hili hakuna kwa insurance yoyote hapa nchini
3. Mwanachama anapata huduma kwenye vituo zaidi ya 8,000 vilivyosajiliwa nchi nzima yeye na wategemezi wake
4. pamoja na huduma za kawaida .....mwanachama atapata huduma za matibabu ya cancer, dialysis, pamoja na huduma za magonjwa yasiyo ambukiza kama vile kisukari, pressure n.k na hii wanapewa dawa kila mwezi kwa kutumia NHIF.
Mambo mengi hapo huwezi kuyapata kwenye Bima binafsi kwa sababu wao wanajiendesha kibiashara.....They are doing FUND MANAGEMENT yaani unawapa fedha yako wakushikie ukipata shida ya Afya wanakulipia then zikiisha unaambiwa ongeza nyingine BUT
NHIF ni social health insurance ambayo unachangia kulingana na uwezo wako.... na unapata huduma za matibabu kulingana na janga lililokupata bila kujali ulichangia nini. .....Ndani ya NHIF UNATUMIA kulingana na kilichoandikwa na daktari.
HIVYO NI MUHIMU WATANZANIA tukawa tunapenda vitu vyetu......nikimaanisha kwamba kama kuna shida tutoe maoni yashughulikiwe lakini tusilalamike kana kwamba hakuna linalofanyika. Watanzania wengi waliopata matatizo wanajua umuhimu wa NHIF.