NHIF mnaumiza wanachama wenu

Status
Not open for further replies.

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,284
2,000
Mimi kama mtanzania wa hali ya chini naomba nitumie fursa ya kuwasilisha machache kuhusu NHIF -mfuko wa bima ,chakushangaza na kusikitisha nhif umeondoa baadhi ya dawa katika orodha yenu ya madawa kwa wanachama huku mkijua gharama ya dawa ni kubwa mno mtaani lakini ajabu zaidi michango ya wanachama iko pale pale. Mfano mmoja wa hizo dawa ni injection iron sulphate, ambayo bei ya mtaani ni Tshs 9000 mpk 15000. Hii inaumiza mno. Tu naomba liangaliwe
Nhif ni mradi wa kukusanya hela kwa wafanyakazi na wananchi wenye kipato cha kati. Gharama za ni kubwa kwa mwananchi wa kawaida. Kwa watu wazima 60+ ni kama hawatakiwi kuwa na bima.
 
KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,901
2,000
Huo ndio ukweli kuwa NHIF ni wezi wa mchana kwani mtu kama mie nimechangia kwa zaidi ya miaka 35 na nilikuwa siugui kijingajinga leo nimekuwa mzee na kustaafu napatwa na magonjwa yanayoendana na uzee eg Hypertension naandikiwa dawa na specialist ambayo anaona inanifaa lakini ajabu NHIF wametoa waraka kisirisiri kuwa tusipewe hizo dawa na badala yake tupewe dawa za hali yachini zenye low Quality sijui lengo lao tufe mapema? ukirudi kwa Dr anakwambia kuwa bora ununue dawa ambayo amekuandikia kuliko kukupatia dawa zilizopendekezwa na NHIF ....sasa nini hasa maana ya Bima kama hawawezi kufuata maagizo ya Drs wetu? kilichobaki NHIF ni kuibia wateja mchana kweupe
Tafadhali badilisha hapo kwenye miaka 35 ukichangia kwenye mfuko huo.
 
Kashishi yetu

JF-Expert Member
Mar 22, 2014
2,394
2,000
NHIF Pale Hospital ya Wilaya ya Nzega ni hovyo kabisa.

Kazini muda mwingi hawapo!! USIKU PIA HAWAPO!!! JUMAMOSI NA JUMAPILI HAWAPO!!!!

Wagonjwa wanaotumia Bima ni shida tupu!!!

HIVI USIKU ,AU SIKU ZA WIKENDI WAGONJWA WANAOTUMIA BIMA WAMEAGANA NAO KUWA HUWA HAWAUMWI????

Mike wangu alilazwa na mtoto mdogo lakini aliambiwa wahudumu was kujaza Form za NHIF hawapo!!! Hivyo alipie matibabu pamoja na dawa!!! USIKU ule niliwapigia simu watu was Bima! Bahati mbaya wakataka wazungumze na mtu aliyepo Hospitalini!! Mke wangu na ndugu wakashauri ni Bora kulipia mtoto apone maana hali ilikuwa ni mbaya zoezi likashindikana!!!!

Hospital ya Nzega ya Wilaya kitengo Cha BIMA KIMULIKWE VIZURI.

Kadi za kumuandikia mgonjwa unaambiwa kanunue dafutari nje ya pale kwenye geti la kuingilia!!! No biashara ya mtu ile!!!
 
Kashishi yetu

JF-Expert Member
Mar 22, 2014
2,394
2,000
MGURUGENZI WA NHIF MULIKA WATUMISHI WA NHIF HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA.

- Kwanza muda mwingi hawapo kazini.Mfano, JUMAMOSI,JUMAPILI,na nyakati zs USIKU!!! Je WAGONJWA WA BINA NYAKATI HIZO HUWA HAWAUMWI?? NDIVYO MLIVYOAGANA NAO KWAMBA NYAKATI HIZO WAGONJWA WANAOTUMIA BIMA HAWAPASWI KUUMWA NA IKITOKEA WAMEUMWA NYAKATI HIZO WANAPASWA WAJIGHARAMIE MATIBABU ILIHALI WANABI A KISA MJAZAJI WA FORMU HAYUPO KAZINI?????????

-Kadi la Mgonjwa Lile gumu ,Unaambiwa kanunue dafutari dogo hapo getini kwao!!! Huo huenda ni mradi wa mtu.!!

- Dawa nyingi Unaambiwa hazipo kanunue😠Ni wajibu wenu kuhakikisha Dawa zote zipo kwa wagonjwa wa Bima.Vinginevyo mtupage na hela za kununulia HIZO Dawa maduka ya Phamarcy.

MKURUGENZI HAKIKISHA WATUMISHI WAPO MUDA WOTE HASA NYAKATI ZA USIKU NA WIKENDI.HILI NI KEROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,731
2,000
Mkuu kifurushi kinategemea mko wangapi kwenye familia.
Lakini kama mko watatu gharama yake inacheza kuanzia milioni 2.4 kwa class ya chini .......milioni 2.6 kwa class ya katikati .........na milioni 2.9 kwa class ya juu.
Maana kuna sijui bronze, silver na sijui nini.
Tofauti ya hizo bei ni kwamba unataka kwa mfano kwenye sector flani mfano meno coverage iwe kubwa, ya kati au ya chini na vitu vingine vingine
Lakini hicho cha 2.4 sio mbaya kwa maoni yangu.

Kuhusu hao wengine kwa kweli wala sikuhangaika kuwacheki. Tangu napata fahamu zangu nimekua na AAR nimeingiwa taamaa ya NHIF kwa kua mwaka jana waliboresha huduma na mambo nikahisi yatakua ya mamtoni kumbe utopolo juu ya utopolo.
Hao wengine kwa kweli itanibidi niwacheki nikipata mda. Uzuri wa AAR unaingia popote pale. I'm sure Jubilee lazima kina hospital hawataikubali sijui lkn.
Ahsante
 
uncle

JF-Expert Member
Dec 10, 2007
297
250
Wengine tumekata bima za binafsi kukwepa gharama kubwa za dawa za kila mwezi lakini nilipopiga namba yao ya huduma kwa wateja wananiambia ninawalaumu bure, wa kuwalaumu ni wizara ya afya waliowapa muongozo wa kuondoa hizo dawa. 😔
Damn hii serikali kuna vitu vinafanyika vya ovyo sana. Afya ni kitu muhimu sana hawa wanacheza na maisha yetu sasa wizara inawezaje kutoa maagizo ya ovyo namna hiyo
 
mgosani

JF-Expert Member
Dec 25, 2014
936
1,000
Nhif ni mradi wa kukusanya hela kwa wafanyakazi na wananchi wenye kipato cha kati. Gharama za ni kubwa kwa mwananchi wa kawaida. Kwa watu wazima 60+ ni kama hawatakiwi kuwa na bima.
Ukiwa 60+ unalipia laki 9 kwa kundi la bima Timiza na wakati sera ya nchi wenye umri wa miaka 60+ wanatakiwa watibiwe bure! Sasa basi kwanini wasiwekewe kiwango kidogo cha hayo malipo?
 
Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,028
2,000
Ukiwa 60+ unalipia laki 9 kwa kundi la bima Timiza na wakati sera ya nchi wenye umri wa miaka 60+ wanatakiwa watibiwe bure! Sasa basi kwanini wasiwekewe kiwango kidogo cha hayo malipo?
60+ kwa NHIF bei hiyo hapo chini
 
Attachments

  • IMG_20200824_165809.jpg
    File size
    586.2 KB
    Views
    0

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225
Mimi kama mtanzania wa hali ya chini naomba nitumie fursa ya kuwasilisha machache kuhusu NHIF -mfuko wa bima. Ni jambo la kushangaza na kusikitisha NHIF kuondoa baadhi ya dawa katika orodha yenu ya madawa kwa wanachama huku mkijua gharama ya dawa ni kubwa mno mtaani lakini ajabu zaidi michango ya wanachama iko pale pale.

Mfano mmoja wa hizo dawa ni injection iron sulphate, ambayo bei ya mtaani ni Tshs 9,000 mpaka 15,000. Hii inaumiza mno. Tu naomba liangaliwe.
Kwa upeo wangu mdogo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa huduma dawa zote za msingi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, hakuna ukweli wowote wa kuondolewa kwa baadhi ya dawa katika orodha, dawa aina ya intravenous iron sucrose(Iron sucrose Injection) ipo katika orodha ya dawa za NHIF na inapatikana katika hospitali na maduka ya dawa yaliyosajiliwa

zaidi mfuko hivi karibuni kwa kushirikiana na wizara ya afya umeongeza dawa nyingine zaidi 71 katika orodha yake ya dawa hii ni baada ya mapitio na maboresho ya orodha za dawa za msingi zilizoainishwa katika muongozo wa Tiba wa Taifa (Standard Treatment Guideline)
 
Baba wa Mapaka

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
1,394

Kwani lazima uwe na NHIF njoo hata NSSF wako vizuri
 
Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225
Huo ndio ukweli kuwa NHIF ni wezi wa mchana kwani mtu kama mie nimechangia kwa zaidi ya miaka 35 na nilikuwa siugui kijingajinga leo nimekuwa mzee na kustaafu napatwa na magonjwa yanayoendana na uzee eg Hypertension naandikiwa dawa na specialist ambayo anaona inanifaa lakini ajabu NHIF wametoa waraka kisirisiri kuwa tusipewe hizo dawa na badala yake tupewe dawa za hali yachini zenye low Quality sijui lengo lao tufe mapema? ukirudi kwa Dr anakwambia kuwa bora ununue dawa ambayo amekuandikia kuliko kukupatia dawa zilizopendekezwa na NHIF ....sasa nini hasa maana ya Bima kama hawawezi kufuata maagizo ya Drs wetu? kilichobaki NHIF ni kuibia wateja mchana kweupe
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hua unatoa matibabu kwa kufuata utaratibu wa serikali na kuhakikisha kwamba kinachotolewa kwa wananchi kama tiba kimefanyiwa utafiti wa kutosha na kwamba hakina maadhara mengine zaidi ya malengo ya Tiba.

Hivyo dawa za Hypertension zipo kwenye kitita cha NHIF na wewe kama mwanachama unatakiwa kuandikiwa kulingana na jina la dawa la asili. Tatizo tunalokumbana nalo sisi wananchi ni kuwepo kwa baadhi ya watoa huduma ambao siyo waaminifu ambao wanataka kufanya biashara katika miili yetu. Mtu anafanya promotion ya dawa fulani kwa sababu yeye anapata percent kutoka kwa waagizaji.

HILI HALIKUBALIKI ......tuige mfano wa MH. RAISI WETU aliyeweza kupambana na CORONA iliyowashinda mabepari.
 
Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,028
2,000
Kwa upeo wangu mdogo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa huduma dawa zote za msingi kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, hakuna ukweli wowote wa kuondolewa kwa baadhi ya dawa katika orodha, dawa aina ya intravenous iron sucrose(Iron sucrose Injection) ipo katika orodha ya dawa za NHIF na inapatikana katika hospitali na maduka ya dawa yaliyosajiliwa

zaidi mfuko hivi karibuni kwa kushirikiana na wizara ya afya umeongeza dawa nyingine zaidi 71 katika orodha yake ya dawa hii ni baada ya mapitio na maboresho ya orodha za dawa za msingi zilizoainishwa katika muongozo wa Tiba wa Taifa (Standard Treatment Guideline)
Mkuu ulivyoelezea unaonesha unayajua haya mambo vizuri. Ila kumbuka wanaolalamika hapo juu ndi watumiaji halisia wa mwisho wa huduma.

Inaweza kua ulichokisema kiko kwenye makaratasi tu kama maua. Nenda front sasa....utumbo.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom