NHC yambwaga Mbowe Mahakamani

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
Hii inasikitisha sana kwa siasa zetu pamoja na sura halisi ya viongozi wetu
kitaifa. Je Mbowe ni kama Trump kukwepa kodi tangu miaka ya 90?

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameangukia pua mahakamani baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutupilia mbali maombi yake katika mgogoro wake wa umiliki wa jengo la Shirika la Nyumba (NHC).

Mbowe alifungua maombi mahakamani hapo kupitia kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd, akipinga uamuzi wa NHC kumuondoa katika jengo ambalo alikuwa akilitumia kama ofisi ya kampuni yake ya Magazeti ya Free Media na klabu ya Bilicanas.

Katika maombi hayo, pamoja na mambo mengine Mbowe alikuwa akidai kuwa aliondolewa katika jengo hilo jinyume cha sheria kwa kuwa hakupewa taarifa na kwamba kampuni ya udalali iliyotumiwa kumuondoa haijasajiliwa kama dalali wa mahakama.

Hata hivyo katika uamuzi wa mahakama hiyo uliotolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, imetupilia mbali maombi hayo ya Mbowe ikisema kuwa hayana msingi

Jaji Mwangesi alikubaliana na hoja za NHC na akasema kuwa Mbowe aliondolewa katika jengo hilo kisheria.


Chanzo: Mwananchi
 
Mbowe alipe hili deni hakuna namna. Ni mmoja ya waliofilisi mali za umma kwa mgomgo wa upinzani... Lipa sasa. Tatizo Mbowe aliwadanganya vijana wake kuwa lile ni jingo la baba yake...kwa hiyo ni laurithi kama alivyorithishwa chama.Hakuna jinsi ruzuku itatumika kulipia deni hili na ujenzi wa ofisi umeota mbawa.
 
Saafi sana, na akome. Lazima alipe kodi mkwepa kodi mkubwa huyu. Nasikia kaanza kukusanya hela toka kwa wananchi akiwadanganya eti ujenzi wa ofisi kumbe anataka kulipa kodi, hahah
 
Mleta mada mbona unaharaka sana?hebu ivisha kwanza hii habari kwa maana sijaona maneno kama "kwa mujibu wa kifungu namba...,neno katiba nk
 
Mbowe alipe hili deni hakuna namna.Ni mmoja ya waliofilisi mali za umma kwa mgomgo wa upinzani...lipa sasa.Tatizo Mbowe aliwadanganya vijana wake kuwa lile ni jingo la baba yake...kwa hiyo ni laurithi kama alivyorithishwa chama.
Ulivyo na akili ndogo hukawii kudai hadi mama yako mbowe alimrithi ndio mkapatikana nyie na wadogo zako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…