NHC: Tax Exemption & The Never Ending 'Committee' Issue

Napenda kwanza nikushukuru kwa maoni yako na kisha nikuhakikishie
kuwa siyapingi ila nashindwa kukubaliana nawe juu ya hili la kumbandikia lawama Kikwete peke yake binafsi.

Kikwete, amekwisha sema kuhusu Mkapa kwamba kwa vile amwstaafu, tumwachie amani ajipumzikie. Hilo, wewe kama mimi hatukubaliani naye. Hii ni ile ile hulka ya kulindana. "Scratch my back and I'll scratch yours." Hii ni trade mark ya CCM tangu huko ilikotokea TANU na ASP.

Kinachonishangaza ni kuwa Watanzania tumepumbazwa, tumekubali na kuamini kuwa hii serikali tuliyonayo ni serikali mpya ati kwamba hii ni serikali ya Kikwete na ile iliyopita ilikuwa ya Benjamin William Mkapa na kabla yake ilikuwa serikali ya Ali Hassan Mwinyi, aliyerithishwa serikali ya Julius Kambarage Nyerere.

Kwanza hakuna serikali ikawa ya mtu mmoja au ya chama kimoja cha siasa. Siku zote serikali zote duniani zinatakiwa ziwe srikali za wananchi. Iwe wana chama au si wanachama si serikali ni yetu wote, watoto, vijana na wazee. Wanawake na wanaume. Wagonjwa na wazima hali kadhalika.

Tunazugwa kwa kubadilishiwa sura. Serikali inaendeshwa na CCM(TANU na ASP). Sera za CCM ndio hizo hizo tangu Tanganyika ipate uhuru wake 1961 na Afro-Shirazi tangu ifanye mapinduzi yake 1964. Sasa si jui hili la kusema afadhali Kikwete kuliko Mkapa litawezekana vipi. Maziwa ya kisha chacha, hata ukiyabadilishia chupa, yanabaki vile vile kama hayakuharibika zaidi.

Ikiwa kweli wananchi wanaona Nyerere aliharibu, walimchagulia nini Mwinyi na kama naye aliharibu, kwa nini tulimchagua Mkapana baadae huyu tuliyenaye ambae ni Kikwete? Tunaendeshwa na chama ca CCM. Hatundeshwi na Kikwete. Yeye ni alama ya CCM madarakani.

Chama hiki cha CCM kimekuwa madarakani na kuendesha serikali kwa Ilani za chama chao. Kama kinaharibu basi ni sera zao zinaharibu na kama sera, basi utekelezaji mbaya au sera zenyewe hazitekelezeki. Kama hivyo,kwa nini Kikwete asiangushwe hapo 2010
katika Uchaguzi Mkuu 2010. Wanaharibu ni CCM sio watu mmoja mmoja binafsi. Wao hawana sera, sera ni za CCM na hazitungwi na Kikwete au Mkapa binafsi.

Wanaomba muda, muda wa nini na wao weshakuwa madarakani kwa karibu nusu karne hivi sasa?
 
Back
Top Bottom