NHC kuuza nyumba Arusha / Dar es salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NHC kuuza nyumba Arusha / Dar es salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jethro, Oct 18, 2011.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Nimechukuwa muda huu kupenda kujua vyema kuhusu NHC Shirika la nyumba Taifa pale lilipo tangaza kuwa lina uza nyumba zake katika mikoa ya Arusha na Dar -Es-Salaam.

  Kweli katika tangazo lao la wananchi kuandika barua ili kuomba kununua nyumba hapo sawa ila wao NHC hawajatuambia nyumba hizo zinazo uzwa Dar ziko eneo gani au huko Arusha hizo nyumba ziko eneo lipi ni mpya au za zamani?.

  Mashaka yangu makubwa ni kuwa tangazo hilo limetangazwa ni kukidhi majukumu ya kazi kuwa walitangaza nyuma zinauzwa au?

  Tetesi zimeanza kutokeza kuwa nyumba husika zinazo tangazwa kuuzwa tayari kuna vigogo walisha jinyakulia nyumba ili wao waje kuzipangisha kwa raia wengine

  Ni mashaka yangu makubwa kuwa NHC watakuwa hawajatenda haki kwa raia (wakazi wa maeneo husika esp wa kipato cha chini kabisa) kwani siku zote mashirika yetu ya umma yauzapo vitu huwapa vigogo issue then utasikia wametangaza ukifuatiria its toooo late kumbe walisha gawana zamani huko.

  Karibuni kwenye Hoja tujadili
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Ndiyo Bongo hiyo Mkuu jamaa wanataka kujilimbikizia kila kitu wao kama vile Watanzania wengine hawana haki ya kuzinunua nyumba hizo.
   
 3. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu alinijuza huko arusha kuna baadhi ya matajiri tayari walisha pewa nyumba wanasubili tu vibali ili wazimiliki
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  usishangae kusikia riz1 ana mkono wake pia
   
 5. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  usishangae makamba yuko huko pia, manake INJI HII MHHH
   
 6. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shirika la nyumba la Taifa ( NHC ) linahitajika kuuza nyumba mpya ambazo imezijenga na kuzirudisha kwa
  kwa wenyewe nyumba zote zilizotaifishwa wakati wa azimio la Arusha lilipotangazwa mwaka 1966.
  Na kwa ujumla Shirika zima livunjwe, Kwa mfumo tulionao sasa serikali aina dhamana ya kuendesha biashara
  ya aina yeyote ile zaidi ya kuwaongoza wananchi kupanga na kutoa maamuzi ya maendeleo kwa nchi.
  Lakini inashangaza ni kwa nini serikali ya Ccm inang'ang'ania kuwa wakala wa ( Reale Estate )
  Zaidi ya hapo ni ufisadi ambao unaouzidi kuwatia mashaka Watanzania.
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo watu wanashindwa kuelewa serikali yao inashindwa kuhudumia wananchi wake na badala yake imejikita kufanya biashara na kupotea mantiki nzima ya utumishi.

  Mwl. Nyerere Alisema 1995 Mei Mosi - Mbeya "Umaskini wa kufikili ndio umasikini mbaya kuliko umasikini wowote ule dunia" Hicho ndicho chanzo cha matatizo ya viongozi wetu hapa nchini kutokufikili na kujenga hoja na wanatupa majibu mepesi mepesi tuu bora siku ziende
   
 8. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Nyumba zinauzwa milioni 175 na hiyo ni solid cash, je wananchi masikini watawezaje kupata? NHC ni kwa ajili ya wenye nazo hamna sehemu ambayo wanasema watakopesha hizi nyumba kwa wananchi ambao the majority ni masikini, it's just a notion expressed to the mass that NHC housing project is for all tanzanians bila kubagua tajiri ama maskini. In actual sense maskini mil 175 atapatia wapi hiyo ni mshahara wa zaidi ya miaka kumi. NHC msitudanganye
   
 9. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 405
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Sasa tuone watakaonunua nyumba hizo, maana humu jamvini munasema Wahindi ndio wenye kumiliki NHC. Na tungoje, tuangalie huyu mfanyakazi anaeonewa huruma , atazitoa wapi hizo 175m+18% vat, watanunua wafanyakazi wa TRA, tISCAN, Na makamanda katika vita dhidi ya Ufisadi.
   
 10. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NHC ni wezii, tena ni mafisadi wa kubwa, wanauza nyumba milioni 114 pale Dodoma nyuma ya CBE na hizi nyingine arusha milion 175 tena wanataka cash, hivi ni mlalahoi gani atanunua hizo nyumba? hata kama ni mkuu wa wilaya na kimshahara chake cha milion 4 hawezi pata hii cash unless ni mwizi. hapa kuna janja ya nyani yaani naskia hasira sana. kwanin wasiweke mpango wa kuwajengea walim na wafanyakazi wa serikali na kisha kuwakopesha ili kila mmoja apate yake?

  Ivi kama hili toto la JK likiamua kuja kununua nyumba zote anashindwa nn wakati anamiliki bilions of money? hapa wanyonge wanazidi
  kunyongwa na haki zao hawapewi, ipo siku tutajificha porini afu wakipita barabarani tuwatungue na magobore yetu ya asili, inauma sana! anyway Tusizidi kuimbea Tanzania hakika Mungu si athuman anaweza kufanya miujiza wanyonge wakawaongoza wenye nayo.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka kwenye nyumba za Serikali ambazo Mkapa aliamua wauaziane kwa bei ya kutupa baadhi ya Watanzania walitaka kuwe kufanyike mnada ili nyumba zile ziuzwe kwa faida kubwa kwa Serikali, lakini Mkapa na Baraza lake la Mawaziri wakakataa hili kwa kujua kwa kupitia mnada bei ya nyumba zile zingepaa sana na hivyo wengi wao kushindwa kuzinunua. Kama hizi nyumba za NHC zikifanyiwa tathmini sidhani nyingi ya nyumba hizo kutokana na uchakavu zitafika bei hiyo wanayoitaka NHC.

  Kihalali Wafanyakazi wa umma watakaonunua nyumba hizo na kuweza kulipa cash wanatakiwa wachunguzwe wamepata wapi pesa hizo, lakini hili halitatokea pamoja na kauli ya hivi karibuni ya Mkuu wa Kaya kwamba hata watu binafsi wenye mapesa mengi inabidi wachunguzwe kwa kuwa na mapesa mengi, labda wameyapa kupitia biashara ya unga, lakini kama tujuavyo kauli za msanii huwa ni kauli ambazo zinaishia hewani tu na kusahaulika.
   
 12. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Nehemiah kyando mchechu NKM embu tudadafulie hili je kweli itawezekana kwa maskini kuishi kwenye nyumba zenu? dg@nhctz.com
   
 13. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Jamani naona kwa style hii NHC inamalengo mazuri tu,kwa taarifa zilizo rasmi NHC wanataka wauze nyumba zao kwa gharama kubwa ili wapate faida ambayo itawawezesha kutimiza malengo yao ya kujenga majumba maeneo ya dodoma,kigoma na mwanza,na wanataka wao wawe real estate developer wakubwa kwa kujenga nyumba za kisasa....tuendane na mabadiriko ya dunia achaneni na ujamaa.
   
Loading...