Nina wasiwasi na mtoa mada hii juu ya uelewa wake,
1.Namshangaa kupinga Mjumbe wa nyumba kumi hana mamlaka kiserikali na wakati tunashuhudia tatizo likitokea ktk eneo fulani Mjumbe huyu hutafutwa kotolea maelezo/ufafanuzi ikiwemo na hata vyombo vya usalama,pia tunashuhudia wakati unahitaji utambulisho wa makazi kwa matumizi fulani kama mikopo n.k ukifika serikali za mitaa unaambiwa ulete barua kutoka kwa mjumbe wa eneo lako. Je.. hizo ni shughuli za kichama?
2. Ni ufinyu wa fikra kusema CCM inawahonga/kuwa rubuni wananchi kwa mavazi, ila wanacho kifanya CCM ni kusambaza sare za chama kwa manachama,mashabiki na wapenzi wake ukizingatia CCM ina jumuiya nyingi zilizo sambaa hadi vijijini.