Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,139
1.Ujinga-Ujinga wa watanzania walio wengi katika kujua,kufuatilia,kupambanua,na kuelewamambo mbalimbali yahusuyo maisha yao kwa ujumla. Hii ni pamoja na kutojua umuhimu na uzito wa matumizi sahihi ya kadi ya kupigia kura. Pia,wananchi wengi,hadi leo hii,wanaamini kuwa Wajumbe wa Nyumba kumikumi wana mamlaka za kiserikali.Kiukweli,Wajumbe hawa hawana mamlaka yoyote kiserikali isipokuwa ya kichama katika ngazi za mashina. Wajumbe hawa ndio kipumbazio cha juu kwa wananchi wengi wa hasa vijijini.
2.Umaskini-Huu husababisha wananchi kuwa tegemezi. Na ni katika wakati wa uchaguzi,CCM hutumia rasilimali walizonazo kuhadaa wananchi kwa mavazi,pesa na vyakula. Wnanchi hupewa vitu hivi ili kuaminishwa kuwa CCM inawajali,inawapenda na kuwathamini. Wananchi,kutokana na utegemezi wao, hukubali 'zawadi' hizo za wakati wa uchaguzi na kuwachagua wagombea wa CCM.Pia,umaskini huwafanya wananchi kuwa wepesi kupokea kwa moyo mmoja ahadi hata zile ambazo ni za uongo na zisizotekelezeka.
3. Maradhi-Haya huwafanya wananchi kuwa dhaifu,wanyonge na tegemezi. Panaposhamiri jambo hili, wananchi huwaona watu wa CCM waendao hasa wakati wa uchaguzi kama waokozi wao na hivyo kurubunika kirahisi. Maelezo mengine ni kama ya katika umaskini.
Iko wazi,sehemu zenye mambo hayo matatu kwa kiasi kidogo,wananchi huchagua kutokana na utashi wao. Ndiyo maana maeneo ya mijini,CCM hupata upinzani wa nguvu ukilinganisha maeneo ya vijijini ambapo mambo hayo matatu yameshamiri. Itakapotokea mambo hayo yakapungua au kuisha,CCM hawatakuwa na chao.