Nguvu zangu za kiroho zimeenda wapi?

Nguvu zangu za kiroho zimeenda wapi?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,840
Kwa miaka mingi iliyopita nilikuwa ni mtu ambaye naota mambo ya ukweli tu. Nikiota lazima kinatokea, liwe jambo baya au zuri. Ilifika hatua nikiota jambo baya basi nilikuwa sisemi kwa watu, kwa mfano; kuna kipindi mwezi mmoja kabla jirani yangu hajafariki nilikuwa nimeota na kweli ilitokea, marehemu babu yangu kabla hajafariki nilikuwa nimeshaota kabla.

Kuna kipindi ambacho sijawahi kupanda hata ndege miaka hiyo nikaota nipo na safiri na mke wangu tupo nchi za watu na tulipofika huko tumegombana sana. Miezi mitatu baadae ni kweli tulipata safari ya kwenda Canada na kuna ugomvi kweli ulitokea huko. Mara ya mwisho kuota ndoto ya kweli ni 2016 ambapo niliota mke wangu kapata kazi mpya na ni Arusha, ndani ya miezi miwili kweli ikatokea. Lakini baada ya hapo sioti tena ndoto za ukweli. Miaka hiyo naota za ukweli ilikuwa kila baada ya muda fulani naota napaa hewani, hamna ndoto nilikuwa naifurahia kama hiyo. Ni ndoto ilikuwa ikinifanya nijisikie mwili ume relax sana nikiwa hewani na hata nikiamka asubuhi nilikuwa na amani sana.

Maisha yangu ya kipindi hicho, si kwamba nilikuwa mtakatifu. Nilikuwa nikiishi maisha ya kawaida kabisa, kama kudanganya nilikuwa nadanganya kama watu wengine, kuchepuka nilikuwa nachepuka siku moja moja na kanisani nilikuwa siendi. Kwahyo sidhani kama nilikuwa naishi maisha ya kiroho ndiomana ilikuwa hivyo.

Sielewi kabisa kwanini hiyo hali ilipotea kabisa. Kwa ambaye amewahi pitia situation kama yangu tubadilishane mawazo wakuu
 
Kuna mtu amekunyoa "nywele" kama ilivyokuwa kwa samson
 
Anazo jamaa aliyetabiri Mtekwaji atapatikana kabla ya Jumapili.
 
Mkuu imani yako imepungua kabisa ndo sababu ...muamini muumba fuata njia zake atakuonyesha makuu yake
 
Kipawa chako hukukitumia ipaswavyo kimeenda kwa mwenye uwezo!
Kumbuka YESU KRISTO NA TALANTA
 
unaumwa,lakini sitaki kukuambia unaumwa nini usije ukasema uliota mwana JF alikuambia unaumwa..lol
 
Back
Top Bottom