Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,430
NGUVU ZA ZIADA ZINATOKA WAPI?
Nguvu za ziada ni nguvu ambazo baadhi ya binadamu wamebarikiwa kuwa nazo . Huu ni uwezo ambao uko juu ya nguvu za kawaida za WATU . Kwa mfano , mtu kuweza kuona mambo yaliyojificha na kuyasema, au mtu kuweza kuhisi kwamba, jambo fulani litatokea na likatokea kweli . Nguvu za ziada hupatikanaje? Leo hakuna ajuaye ukomo wa nguvu za akili ya binadamu. Mimi binafsi nilikuwa na nguvu za ziada tangu nikiwa na umri wa miaka minane hata leo nazitumia, na uzoefu wangu unaweza pia kuungwa mkono na nadharia ifuatayo.
Imethibitika kwamba, tunatumia asilimia 1.0 tu ya uwezo wa ubongo wetu. Ubongo umegawanyika katika sehemu kuu mbili. Upande wa kushoto ambao huhusiana na mantiki na upande wa kulia unaohusiana na mambo ya ubunifu; upande ambao nguvu za kutengeneza picha ya kitu ambacho kitatengenezwa baadaye kwa mikono unaishi na ni upande ambao nguvu za kulijua jambo kwamba litatokea kwa kuhisi, ndiko ziliko.
Kwa muda wetu mwingi huwa tunatumia upande wa kushoto wa ubongo wetu . Nimegundua kwamba,
tukichanganya ubongo wa kushoto na wa kulia tunaweza kutumia hiyo asilimia 90 ya uwezo wetu kiakili ambao hatuutumii . Upande huu wa ubongo ambao hautumiki ndiko ambako kuna nguvu za ziada na nguvu za kujiponya.
Hii ni nadharia yangu tu . Hata hivyo, tafiti mpya za kisayansi zinakaribia mwanga ambao unaunga mkono nadharia hii. Kama nilivyosema , tukitumia pande zote, tunagusa uwezo wetu ambao tumeuacha bila matumizi. Kwa uzoefu wangu, nguvu za ziada ni tofauti na nguvu za 'machale' , ambayo ni hali ambapo wazo fulani linakuja ghafla na kumwongozoa mtu mahali bora zaidi au kumpa jibu la tatizo Kila mmoja wetu ana nguvu hizi za machale. Isipokuwa kama unataka kuwa na nguvu za ziada, lazima uanzie kwenye kuimarisha nguvu zako za ' machale.
Kwa maana nyingine ni kwamba , nguvu za ziada ni nguvu za juu sana ukilinganisha na nguvu za 'machale' , ambazo nimesema , naamini kila mmoja wetu anazo Kama ilivyo kwa ujuzi mwingine wowote , nguvu za ziada unaweza kufundishwa.
Mazoezi yafuatayo yanaweza kukusaidia kuongeza uwezo wako wa nguvu za ziada. Maana yake ni nini basi?
Ni kwamba, naamini kuwa Si kila mmoja kati yetu ni mwenye nguvu Hizi, lakini kila mmoja unaweza kujifunza kuwa nazo.
Kwanza ni kufanya tahajudi kwa Kutumia njia mbali mbali mpaka utakapopata aina aina moja ya tahajudi ambayo utaiona muafaka kwako.
Kumbuka hakuna aina bora ya tahajudi kuliko nyingine.
Bali kila mmoja unaweza kukuguswa Vizuri na Kwa manufaa zaidi na njia moja ya tahajudi kuliko nyingine.
Pili jaribu kuyaelewa mazingira yako. Unapoamka asubuhi, fanya juhudi ya kuendelea kujilaza kitandani kwanza, huku ukiwa umetulia kwa dakika chache bila kufunga macho.
Jaribu kuchunguza sauti nyingi na harufu mbali mbali nyingi kwa kadiri uwezavyo, kabla hujafunga macho yako.
...... Ukiyafanya mazoezi hayo kwa wiki kadhaa yanaweza kukuongezea kwa kiasi kikubwa kusaidia viwango vya kutambua na kuweza kuhisi mambo yanayoweza kutokea.
..... Tatu, sikiliza. Kitendo cha kusikiliza ni muhimu sana katika kuongeza nguvu za juu za kutambua.
Baada ya kuendelea na zoezi hili kwa kipindi fulani , utaanza kugundua ongezeko la kutambua kwa ujumla wake ambao ni mwelekeo sahihi wa kuelekea kwenye nguvu za kuhisi mambo yatakayotokea Tilia umuhimu kufikiria mambo mbalimbali.
Tunza daftari ambalo utatembea nalo muda wote, na jaribu kuandika mawazo ambayo yanaonekana kukujia kutoka kusikojulikana Utagundua baada ya muda kwamba mtiririko fulani unajitokeza. Mawazo ambayo mwanzoni yalionekana kwamba hayako katika mpango fulani yanaanza kutengeneza wazo linaloeleweka.
Nakili ndoto zako kwenye daftari. Ni rahisi kukumbuka ndoto zako.
Jipe muda kidogo wa kutulia baada ya kuamka usingizini ili iwe rahisi kuzikumbuka ndoto zako.
Mazoezi haya mepesi yanaweza kuleta matokeo ya ajabu kama yakifanywa mara kwa mara. Ili kujenga nguvu za zinda lazima ujiamini na lengo lako liwe la heri.
Bujibuji