Nguvu za imani za kichawi na hatma ya siasa zetu

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
1570705291557.png
Ijapokuwa hakuna takwimu za kisayansi mezani; Imani za Uchawi ni jambo lenye nguvu sana katika siasa za nchi nyingi za kiafrika. Nasi tukiwa kama sehemu ya bara la Afrika, tumekuwa tukiathiriwa vibaya na nguvu za imani za kichawi kwenye siasa zetu kwa kipindi kirefu na hali hiyo inatarajiwa kuendelea kama jambo hili litabakia kama lilivyo.

Pamoja na kwamba jambo hili halizungumzwi sana , pengine kwa kuwa hamna tafiti ,ushahidi wa moja kwa moja wa uwepo wake au kupuuzwa lakini ni jambo linaloaminiwa na watu wengi hasa katika ulingo wa siasa zetu. Ipo idadi kubwa ya watu wanaoamini kuwa ni vigumu kupata mafanikio ya kisiasa bila kutumia uchawi. Kwa lugha nyingine, inaaminika miongoni mwa wadau kuwa kwa kupitia uchawi unaweza kupata nafasi ya kisiasa, kujenga ushawishi n.k. Vile vile unaweza kudhibiti wenye maoni tofauti na yako kiuchawi uchawi.

Chakushangaza zaidi, inaonekana imani hii ipo miongoni mwa vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume, wasomi na wasio wasomi.

Hebu jaribu kufiki mtu ana degree, Masters au hata PHD lakini anaamini kwamba siri ya mafanikio au kutofanikiwa ni uchawi, na huyo ndie mdau wa siasa na mwisho anakuwa kiongozi wa wengine, maana yake ndie anayeonesha au anatarajiwa kuonesha njia wengine .

Inaweza kuwepo mantiki ikiwa, mtu atajenga hoja ya kwamba; moja ya sababu zinazotusababisha tuwe nyuma kimaendeleo karibu kwenye kila jambo ni imani ya hali ya juu kwenye uchawi kiasi kwamba tunaamini kwamba mtu hawezi akawa mwanasiasa au kiongozi akafanikiwa bila uchawi na pia njia ya kwanza ya kuaminika ya kushinda wengine ni uchawi na kwa mantiki hiyo siri ya mafanikio ni uchawi.

Mtu anaweza kuhoji, kwamba anayeandika haya anatumia hisia au? Lakini atakayeuliza swali hilo akili yake mwenyewe itakuwa inampa majibu ya hiki hiki kilichoandikwa hapa. Kwa mfano ni kitu cha kawaida kumuona mdau wa siasa akifanya matukio ya kichawi hadharani (achilia mbali yanayofanyika sirini)au angalau hata unaweza kusikia mwingine akilalamika anavyosumbuliwa na wachawi kwa sababu ni kiongozi kwenye eneo fulani au anataka kuwa kiongozi au ana maoni Fulani kuhusu jambo Fulani.

Kwa mantiki hiyo, wakati mwingine unaweza kuona kiongozi huyu ama yule anafanya kitu kisicho cha kawaida ukajiuliza mbona kawa hivi? Kumbe keshalogwa tayari hahahhahahahah. Au kaloga mtu lakini kwenye kufanikisha hilo masharti yalikuwa makali na kila akiyakumbuka inakuwa tabu.

Tunaweza kusema, itakuwa ni vigumu sana kupiga hatua za maana kama bado tutaendelea kuwa na wanasiasa au wadau wa siasa ambao wanaamini msingi wa mafanikio ni uchawi.Ikumbukwe mwanasiasa ndio kiongozi na siasa ndio huamua nani apate nini, kivipi, wapi ,sangapi, kwa nini na kipi kiwe wapi na kiweje.

Kwa kuwa wanasiasa na wadau wa siasa ni zao la jamii; ni sawa na kusema imani yao ni taswira ya imani ya jamii yetu katika upana wake. Kwa hiyo ili tuweze kufanikiwa, inatupasa kwanza tuamue kubadili mtizamo wetu juu ya mambo haya. Vinginevyo labda kizazi hiki kitakapo isha na kuja kizazi kingine, lakini hicho kizazi kingine hakiwezi kuwa bomu kuliko hiki cha kwetu?
 
Mtazamo wangu ni kwamba swala la watu hasa wanasiasa kujiingiza na ushirikina hii inatokana na sisi waafrika walio wangi kuamini kwamba mafanikio hayaji kirahisi, na hii ndio hupelekea wengi kujiingiza kwenye ushirikina.
 
Jambo kama hili linaweza kuonekana kama mzaha ila kiuhalisia jambo lolote kabla ya kufanyika linakuwa ni wazo ndani ya kichwa cha mtu.

Kwa hiyo mambo yanayofanyika au yatakayofanywa hutegemea na vile watu wanavyofikiri.Imani ndio hutoa muelekeo wa namna ya kufikiri.

Sasa fikiria katika mazingira ambayo unaweza ukajikuta watu wanaotakiwa waamue juu ya Maisha yako, wanaamini msingi wa kufanikiwa au kutofanikiwa ni uchawi. (iwe wewe unaamini hivyo pia au vinginevyo)

Na tatizo zaidi ni kwamba msingi wa Imani ya uchawi sio kumfanya anayeutumia afanikiwe, bali kuwadhibiti wengine wasifanikiwe. sasa katika jamii ya namna hiyo tunategemea nini kitokee?
 
Kuna rfk yangu mbunge japo kwa sasa alishatemwa alikua ananisimulia jinsi walivyokua wanalala makaburini wanavuka ziwa usiku sijui wanalala juu ya miti n.k kwa kweli nilimshangaa sana na usomi wote anaongozwa na fikra potofu hivyo. Ndo maana huwezi shangaa kipindi cha pili hakupita kwa sbb aliamini ushirikina ndo ulimpitisha. Haya mambo siyaelewi labda kwa sbb sijawahi jaribu labda nikijaribu kuloga siku moja ntayaelewa.
 
Imani hizi potofu japo wengi wanazitumia, ila wapo viongozi wa kisiasa ambao wamefanikiwa bila uchawi
 
Jambo kama hili linaweza kuonekana kama mzaha ila kiuhalisia jambo lolote kabla ya kufanyika linakuwa ni wazo ndani ya kichwa cha mtu.

Kwa hiyo mambo yanayofanyika au yatakayofanywa hutegemea na vile watu wanavyofikiri.Imani ndio hutoa muelekeo wa namna ya kufikiri.

Sasa fikiria katika mazingira ambayo unaweza ukajikuta watu wanaotakiwa waamue juu ya Maisha yako, wanaamini msingi wa kufanikiwa au kutofanikiwa ni uchawi. (iwe wewe unaamini hivyo pia au vinginevyo)

Na tatizo zaidi ni kwamba msingi wa Imani ya uchawi sio kumfanya anayeutumia afanikiwe, bali kuwadhibiti wengine wasifanikiwe. sasa katika jamii ya namna hiyo tunategemea nini kitokee?
Mbona umerudia kilicho andikwa na muanzisha Thread
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom