Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Pamoja na kwamba jambo hili halizungumzwi sana , pengine kwa kuwa hamna tafiti ,ushahidi wa moja kwa moja wa uwepo wake au kupuuzwa lakini ni jambo linaloaminiwa na watu wengi hasa katika ulingo wa siasa zetu. Ipo idadi kubwa ya watu wanaoamini kuwa ni vigumu kupata mafanikio ya kisiasa bila kutumia uchawi. Kwa lugha nyingine, inaaminika miongoni mwa wadau kuwa kwa kupitia uchawi unaweza kupata nafasi ya kisiasa, kujenga ushawishi n.k. Vile vile unaweza kudhibiti wenye maoni tofauti na yako kiuchawi uchawi.
Chakushangaza zaidi, inaonekana imani hii ipo miongoni mwa vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume, wasomi na wasio wasomi.
Hebu jaribu kufiki mtu ana degree, Masters au hata PHD lakini anaamini kwamba siri ya mafanikio au kutofanikiwa ni uchawi, na huyo ndie mdau wa siasa na mwisho anakuwa kiongozi wa wengine, maana yake ndie anayeonesha au anatarajiwa kuonesha njia wengine .
Inaweza kuwepo mantiki ikiwa, mtu atajenga hoja ya kwamba; moja ya sababu zinazotusababisha tuwe nyuma kimaendeleo karibu kwenye kila jambo ni imani ya hali ya juu kwenye uchawi kiasi kwamba tunaamini kwamba mtu hawezi akawa mwanasiasa au kiongozi akafanikiwa bila uchawi na pia njia ya kwanza ya kuaminika ya kushinda wengine ni uchawi na kwa mantiki hiyo siri ya mafanikio ni uchawi.
Mtu anaweza kuhoji, kwamba anayeandika haya anatumia hisia au? Lakini atakayeuliza swali hilo akili yake mwenyewe itakuwa inampa majibu ya hiki hiki kilichoandikwa hapa. Kwa mfano ni kitu cha kawaida kumuona mdau wa siasa akifanya matukio ya kichawi hadharani (achilia mbali yanayofanyika sirini)au angalau hata unaweza kusikia mwingine akilalamika anavyosumbuliwa na wachawi kwa sababu ni kiongozi kwenye eneo fulani au anataka kuwa kiongozi au ana maoni Fulani kuhusu jambo Fulani.
Kwa mantiki hiyo, wakati mwingine unaweza kuona kiongozi huyu ama yule anafanya kitu kisicho cha kawaida ukajiuliza mbona kawa hivi? Kumbe keshalogwa tayari hahahhahahahah. Au kaloga mtu lakini kwenye kufanikisha hilo masharti yalikuwa makali na kila akiyakumbuka inakuwa tabu.
Tunaweza kusema, itakuwa ni vigumu sana kupiga hatua za maana kama bado tutaendelea kuwa na wanasiasa au wadau wa siasa ambao wanaamini msingi wa mafanikio ni uchawi.Ikumbukwe mwanasiasa ndio kiongozi na siasa ndio huamua nani apate nini, kivipi, wapi ,sangapi, kwa nini na kipi kiwe wapi na kiweje.
Kwa kuwa wanasiasa na wadau wa siasa ni zao la jamii; ni sawa na kusema imani yao ni taswira ya imani ya jamii yetu katika upana wake. Kwa hiyo ili tuweze kufanikiwa, inatupasa kwanza tuamue kubadili mtizamo wetu juu ya mambo haya. Vinginevyo labda kizazi hiki kitakapo isha na kuja kizazi kingine, lakini hicho kizazi kingine hakiwezi kuwa bomu kuliko hiki cha kwetu?