Nguvu ya umma

ntemi masali

Senior Member
Joined
May 20, 2013
Posts
136
Reaction score
26
Tunapozungumzia "nguvu ya umma" tunamaanisha watu wanapoikosa haki yao kutoka kwa watawala na kuamua kujikusanya pamoja na kuidai haki hiyo kwa nguvu wakiwa wamoja .Watanzania sasa wameshaamua kudai haki zao kwa kutumia umoja wao yaani NGUVU YA UMMA kama wanavyoonekana hapa. kuna tetesi kuwa CCM nao wanatamani kupata watu wengi kama hawa kwenye mikutano yao bila kuwasomba kwa maloli na kuwapa chakula na soda mkutanoni eti wanauliza wafanyaje ?? wana janvi wapeni ushauri. View attachment 109048
 
Umma huo wote umejiandikisha katika daftari la wapiga kura???
 
waache ufisadi,kumwagia watu tindikali, kurusha mabomu kwenye mikutano ya cdm, waache ujangili kama unaoongozwa na kinana, waache kudanganya uma kua wametekeleza ahad wakati hawajafanya ki2 kama mwigulu,
 
Yaani kama wakiamua kurudisha raslimali zetu zote, na mapesa waliyoficha Uswiss, kusaini mikataba upya ya madini, kuwakamata wote waliotajwa kwenye kashfa za pesa za EPA, MEREMETA, RICHMOND, na yale majina aliyo nayo Mkulu wa Kaya ya Wafanya biashara ya unga, na yule jamaa wa kuua Tembo wetu na kusafisha kwenye zile meli, "Walahi wanini wadhei mie nahamia CCM sasa hivi.
 
Hakuna namna yoyote ya kufufua waliokufa ndugu , muda wa ccm kufanya hivyo umekwenda ! Hakuna haja ya kupoteza muda kuwashauri .
 
wabadilike...ila sijajua badiliko la maiti ni lipi?
 
Hakuna njia itakayoiwezesha CCM kukusanya watu namna hii tena, maana hata wakusombwa kwa malori na kupewa ubwabwa wameshindwa kuwapata.

Labda kwa ushauri wangu ccm wajiite CHADEMA B, labda hapo wanaweza kupata watu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hizi Nyomi huwa nazifananisha na zile za Kule Kenya wakati wa kampain

 
Ccm ata wagawe kanga t shirt na pesa na wasanii wao wote awawezi kujaza ivi
 
Kweli CCM inakaribia kufa kifo cha mende (miguu juu). Wananchi tumechoshwa na kutokuwa na mwelekeo toka 1967 baada ya Azimo la Arusho.
 
Kwa hisani ya Ntemi masali

Peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
ccm jiandaeni kuondoka madarakani, wauza unga na mafisadi wakubwa
mmetufikisha hapa tulipo


 
Hivi kweli na viongozi wa ccm wanaziona hizi nyomi, wallah ccm inaelekea kufa na ndiyo maana kwa sasa ukiwa diwani au mbunge wa ccm fanya uzalendo na wapinge kwa nguvu na tetea wananchi kadri uwezavyo maana hawana ubavu wa kukufukuza uanachama ref madiwani wa bukoba. viva uongozi thabiti wa chadema. Naomba watu km akina nape,nchemba,lusinde,serukamba,kinana,mangula nk wajaribu kuhudhuria mikutano ya cdm wajionee jinsi chama kinavyokubalika.Pia wabunge wetu jiandaeni kwa manyanyaso hapo bungeni yanayofanywa na kiti cha spika maana bunge ni kesho kutwa, hata mkinyanyaswa kiasi gani sisi tuko upande wenu cha msingi msimamie hoja kwa maslahi ya taifa, naomba pia muwashawishi wabunge km filikunjombe, kangi lugora, mpina, esta bulaya, abdalah mtutura wasaidie kuisimamia serikali na si kuitetea. Ni mtazamo wangu tu.
 
Jeshi la polisi na usalama wa Taifa wapo busy na chadema, ndiyo maana majambazi wapo huru.... Nguvu zote wanazotumia polisi na usalama wa Taifa unatokana na biashara ya Unga. Fedha za Unga inawawezesha dola kuvunja sheria

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwa hisani ya Ntemi masali

Peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
ccm jiandaeni kuondoka madarakani, wauza unga na mafisadi wakubwa
mmetufikisha hapa tulipo


mkuu unafikiri arusha kusingerushwa bomu hapa ingekuwaje?
 
Kabla ya uchaguzi kuna utaratibu wa kujiandikisha kwa hiyo usihofu mkuu!

Mkuu 2010 watu hawakuandikishwa ila walihakikiwa tu

ila endepo daftari la wapiga kura litaandikwa upya ccm kwa heri.

maana inasemekana nusu ya wapiga kura Wapo nje ya daftari hasa vijana.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…