Nguvu ya umma yavinyima usingizi vyama vya siasa nchini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya umma yavinyima usingizi vyama vya siasa nchini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FMuhomi, Dec 5, 2011.

 1. F

  FMuhomi Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Inasemekana kuwa nguvu ya umma imekuwa ikivinyima usingizi vyama vya siasa nchini: 1).CCem imekuja na sera ya kujivua gamba ili irejeshe imani kwa wananchi 2).Nccra imekuja na dhana ya kumng'oa mwenyekiti wao Jamus kwa kile kinachoelezwa na wabunge wake wawili wa Kigoma kuwa ni kibaraka wa CCem 3).Mtafaruku wa viongozi wa juu kabisa wa CaFu, bwana Maalim na Hemedi juu ya kuzorota kwa chama chao Tanzania Bara na dhana ya ndoa na chama tawala. Haya yote yanajiri nyakati hizi ambazo dhana ya nguvu ya umma imeshika hatamu na wananchi wa Africa kujitambua kifikra.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nguvu ya umma ya kweli inapaswa kuogopwa na serikali yoyote, hata ikiwa na jeshi kubwa kiasi gani, ila Tanzania nguvu ya umma ya kweli bado kwa sababu ya woga. Kwanza nawapongeza Chadema walioonesha njia katika kutafuta haki kwa njia mbalimbali ikiwepo nguvu ya umma. Nawapongeza pia wananchi wengi waliounga mkono kudai haki bila woga, hata wengine kupoteza maisha yao kwa nyakati mbalimbali: Arusha na Igunga Mungu awalaze mahali pema, awape thawabu wanayostahili, awasamehe makosa yao yote, hasa baada ya kuwa tayari kutoa maisha yao kwaajili ya ukombozi wa mtanzania.
  Tanzania bado kuna haja kubwa ya wananchi- nguvu ya umma zaidi kuamka. Nguvu ya umma haitazuiwa na kitu chochote, kama alivyosema kamanda Lema hata risasi haitaweza. Wapo watakaokufa, wapo watakaojeruhiwa na hata kuwa vilema, lakini mwisho wa yote haki itapatikana kwa watanzania wote. Hiyo ndiyo itakuwa siku ya furaha kuu, siku serikali dhalimu itakapotolewa madarakani, siku risasi za polisi zitakaposhindwa kuua nguvu za umma, siku mtanzania wa kawaida atakapoanza kufurahia matunda ya kweli ya uhuru wa nchi, siku mafisadi wote watakapofikishwa mbele ya sheria na haki itakapotendeka, siku mali yote ya mafisadi waliyopata kwa njia za kifisadi zitakapotaifishwa na hela hizo kuelekezwa katika miradi ya maendeleo kama vile hospitali, mashule, maji, umeme. Siku ambapo wawekezaji watalazimika kuitendea haki nchi yetu kwa kulipa mrabaha wa haki kwa kile wanachovuna katika ardhi yetu. Siku ambapo ukoloni mamboleo utakapokuwa msamiati wa past tense. Naam hiyo siku tunayoitamani iwadie. Hakika tunaamini hiyo siku itawadia kabla kizazi hiki hakijapita.
  Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki juhudi zote za kuitoa serikali dhalimu na mafisadi madarakani, Mungu ibariki juhudi zote za kumrudishia utu mtanzania.
   
 3. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Oya jifunze kuandika vizuri...
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Hapo kwa CUF sosi ya ugomvi wao ni Bakwata (Hamad Rashid) dhidi ya Sunni (Seif Shariff Hamad)
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha bakwata ni shia au?
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Nguvu ya Umma inawafanya CCM wavuane nguo mbele ya watoto..
  I looove nguvu ya Umma..!
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Najiuliza tu sidhhani kama watafanikiwa kugain tena trust ya watz ambao kila kukicha wanapoteza matumaini ya kuishi.
   
Loading...