Nguvu ya UMMA ya TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya UMMA ya TANZANIA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kigu, May 27, 2012.

 1. k

  kigu Senior Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa, 2jue nn maana ya NGUVU YA UMMA?
  kwa vyoyote utakavyo itafsiri "nguvu ya umma" mfano wake mzuri unaweza kuchukua tukio lililo pelekea aliekua rais wa Misri Husni Mubarak, KUJIUZULU , sababu ya kujiuzulu ni "nguvu ya umma" wananchi wengi wa Misri hawamkubali Mubarak, hivyo wakaamua kujitoa kwa lolote ili Mubarak atoke ikulu, pamoja na kupata upinzani kutoka kwa vyombo vya dola baadhi ya wananchi kuuliwa na polisi, lakina hawakurudi nyuma mpaka wamefanikiwa, na mifano mingine mingi ambayo inahusiana na nguvu ya umma.

  Turudi na "Nguvu ya umma ya Tanzania"!!, nguvu ya umma kwetu hapa huwa inatumika ktka sehemu tofauti tofaut kwa lengo la kuleta mabadiliko, yakiongozwa na baadhi ya wanasiasa we2 wa vyama vya upinzani, lakini hatujawahi kupata hayo mabadiliko tunayo yataka ingawaje watanzani wenzetu hupoteza maisha ktk harakati hizo za "nguvu ya umma", kwa mfano huko Zanziba ambako ndugu zetu walikufa na wengine mpaka leo wana majiraha ya risasi katika maandamano ya kupinga ushindi wa Karume(mtoto) na kutaka uchaguzi urudwe,matokeo yake ni kwamba Karume aliendelea kuwa Rais wa Zanziba na uchaguzi haukurudiwa, yakaja mambo ya muwafaka kati ya CUF na CCM na mazungumzu kati Maalim Seif na Karume.........

  Tukienda Arusha, nako nguvu ya umma ilitumika kupinga uchaguzi wa meya,kwa madai kuwa taratibu zilikiukwa, na kumpinga meya mwenyewe kuwa hawamtambui, .....mwisho wa siku watu walipoteza maisha wengine wanatembea na risasi, mpaka sasaiv meya bado ni yuleyule na hakuna mabadiliko, nasikia kuna mazungumzo yanaendelea kati ya chadema na serekali kuhusu tatizo la meya arusha..........


  NGUVU YA UMMA TANZANIA WAPI TUNAKOSEA
  .........?
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwandishi hebu badili rangi ya maandishi yako bana.
   
 3. s

  suli Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  we jamaa ndo rang gani hyo ulotumia? hujui kuwa inaumiza macho tu?
   
Loading...