Uchaguzi 2020 "Nguvu ya umma" itaamua uchaguzi huru na haki mwaka huu

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametoa wito kwa kila mwanachama wa Chadema mwenye sifa za kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais, Ubunge, Uwakilishi au Udiwani achukue fomu za kuwania uteuzi ndani ya chama.

Katibu Mkuu Mhe. Mnyika ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya ratiba ya shughuli ya uchukuaji, utafutaji wadhamini na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na Uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kuanza rasmi hapo jana Jumamosi Julai 4, 2020.

Aidha, Mhe. Mnyika amewataka wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama vyao kuhakikisha mgombea aliyeshinda uchaguzi anatangazwa kwa kutumia nguvu ya umma.

Katibu Mkuu Mhe. Mnyika amesema kwamba imejengeka desturi kwa Wakurugenzi na Wasimamizi wa Uchaguzi kuchakachua matokeo na kumtangaza mtu ambaye hakushinda uchaguzi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria, halikubaliki na linastahili kupingwa kwa nguvu ya umma.

"Natoa wito kwa wanachama hata wale ambao hawakutia nia waende kwenye ofisi za chama wakachukue fomu.

"Kutia nia ni jambo moja na kuchukua fomu ni jambo jingine. Kwa ujumbe huu nawataarifu wanachama wote kutumia fursa hii ili mteuliwa muende kuwahudumia wananchi," amesema Mhe. Mnyika alipokuwa akifungua Mkutano wa Semina ya Watia nia wa Ubunge katika majimbo 19 ya Kanda ya Pwani, iliyofanyika jana katika Hoteli ya Lions, jijini Dar es Salaam.

"Aidha, natangaza rasmi kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi wa nguvu ya umma. Wananchi wakapige kura kwa wingi wao na wahakikishe wanalinda ushindi wao kuanzia kwenye vituo vya kupigia kura mpaka kwenye vituo vya kujumlisha matokeo," amesisitiza Mhe. Mnyika.

Kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Singo Kigaila, Katibu wa Kanda ya Pwani, Hemed Ali akitoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, alisema jumla ya wanachama 148 wametia nia kwenye nafasi ya ubunge kwenye majimbo 19 katika kanda hiyo na wengine 691 kwenye nafasi ya udiwani.

Imetolewa leo Jumapili Julai 5, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
 
Uchaguzi wa mwaka huu una tofauti gani na wa mwaka 2015 linapokuja suala la tume ya uchaguzi na issue nzima ya utangazaji matokeo? Kuna jipya?

It might be worse. CHADEMA mnapaswa kujipanga kwelikweli. The so called “nguvu ya Umma” (kama ya 2015!?) most likely ikazimwa na nguvu ya dola kama mtaendelea kuomba na kutegemea huruma ya tume na/au wapiga kura.
 
Uchaguzi wa mwaka huu una tofauti gani na wa mwaka 2015 linapokuja suala la ya uchaguzi na issue nzima ya utangazaji matokeo? Kuna jipya?

It might be worse. CHADEMA mnapaswa kujipanga kwelikweli. The so called “nguvu ya Umma” (kama ya 2015!?) most likely ikazimwa na nguvu ya dola kama mtaendelea kuomba na kutegemea huruma ya tume na/au wapiga kura
Uchaguzi wa mwaka huu una tofauti kubwa ukilinganisha na wa mwaka 2015......

Kwa kuwa uchaguzi wa mwaka huu, hao CCM wameamua kufanya "wizi" wa waziwazi kabisa, kwa kutumia vyombo "vyao" vya dola
 
Kwa kutumia nguvu ya Unma, ndiyo njia pekee ya kukabiliana na hao CCM, ambao wao wanaamini kuwa vyombo vyote vya dola viko upande wao
Nguvu ya umma gani? Umma wa watanzania tunajua nyie ni matapeli wa kisiasa. Wapinga maendeleo ya watu na taifa letu.
 
Mbona sikusikii ukitia Nia Kyela, Unamuogopa Dr Hunter Mwakifuna?
Masahihisho : Hunter Mwakifuna ni clinical officer , siyo Daktari . kwa taarifa yako ni kwamba akisikia nimechukua fomu anaweza hata kukimbia kyela , hata hivyo mimi nimetia nia ya kuomba uteuzi wa chama changu , si mgombea per say ikiwa kama nitateuliwa na chama basi bila shaka utanisikia
 
Nguvu ya umma gani? Umma wa watanzania tunajua nyie ni matapeli wa kisiasa. Wapinga maendeleo ya watu na taifa letu.

Wewe Mataga nani aliyekupa mamlaka ya kutusemea sisi Watanzania? Kwani nyinyi Ccm mna faida gani kwenye nchi hii zaidi tu ya kuendekeza vitendo vya rushwa, ufisadi, upendeleo, wizi wa mali za umma, kununua wanasiasa uchwara kwa kodi zetu na kujilimbikizia mali?
 
Back
Top Bottom