Nguvu ya nyota na sifa zake

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,479
5,068
6ee9b2c3c014f43c56a133af2a870708.gif
19edbb3b43a350445a52c7019750d50c.gif
cc9ef5ac8b900a80a2102d39d8f7b6b3.gif
2590a52f166fc4a38916e0a1ceff1fe5.gif
0046403369272a4ba676b5637dcc5dc7.gif
2dce9a1ac56002fb6027dbdfebee231d.gif
f32fc683c7893339aba731ae7abedf64.gif
d1b9fd6c029bfa6b3e6728011cad5fbd.gif
44730569d37ebde101fc20e474c29fab.gif
05d848c5618b1c1d1bd97ab11df87ebc.gif
ba8ce1787824811980dde618b2aa6333.gif
83d7fc666c45bf97905d794fe75b0637.gif
7c0128e7fc1141f8d94c3bc721ea0a01.jpg


Unajimu au astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani. Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.

Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi. Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.

Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.

Soma pia:
Madhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli?
Nyota na Kazi Zenye Mafanikio
Tabia za Watu na Alama za Nyota

Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.

Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:

1. Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20
2. Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19
3. Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21
4. Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20
5. Kaa (Cancer): Juni 21 – Julai 22
6. Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22
7. Mashuke (Virgo):Agosti 23 – Sept 22
8. Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22
9. Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21
10. Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21
11. Mbuzi (Capricorn):Des 22 – Jan 19
12. Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

Makundi ya Alama za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:
Moto: Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
Maji: Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
Hewa: Imara na yenye kukuza au kuendeleza
Udongo: Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha

Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani. Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:

Moto : Kondoo, Simba,Mshale
Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi

Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:
Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”: Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
Yenye Kubadilika “Mutable”:
Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
Isiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki

Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama

Kondoo
Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.

Haiba na Tabia za Alama za Nyota

#1 Nyota ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19
Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
Kiongozi
Muongeaji
Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
Mwaminifu kwa marafiki na familia
Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi

#2
Nyota ya Ng’ombe: Aprili 20 -Mei 20
Ni alama ya udongo:
Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
Makini na muangalifu
Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
Mstahimilivu
Mwenye kutegemewa
Ni mgumu kubadilika
Anapenda vitu vizuri na vya thamani
Unapenda urembo na vitu vya kupendeza
Mwenye hisia zilizofichika
Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.

#3 Nyota ya Mapacha: Mei 21 – Juni 20
Ni alama ya hewa:
Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
Anafikiri kwa haraka na mcheshi
Ni mwasilianaji mzuri
Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
Hana utulivu
Ana mipango na malengo makubwa
Mwenye kubadilika kirahisi

#4 Nyota ya Kaa: Juni 21 – Julai 22
Ni alama ya maji:
Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpa utulivu, usalama na amani
Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
Ana huruma
Ni mwangalifu
Mkimya na

#5 Nyota ya Simba: Julai 23 – Agosti 22
Ni alama ya moto:
Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.
Anapenda kuonekana na watu
Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
Mwenye matumaini mazuri
Mwenye kuheshimika
Mshindani
Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
Mwenye mvuto

#6 Nyota ya Mashuke: Agosti 23 – Septemba 22
Ni nyota yenye alama ya udongo
Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
Wanajali afya

#7 Nyota ya Mizani: Septemba 23 – Oktoba 22
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.
Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.
Husimamia haki na usawa
Anapenda sanaa na urembo
Wabunifu wa sanaa
Ni mpenzi wa muziki
Ni muwazi katika kuonyesha upendo
Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
Mpenda amani
Wenye mvuto wa kupendwa

#8 Nyota ya Ng’e: Oktoba 23 – Novemba 21
Ni alama ya nyota ya maji na ni mwenye hisia nzito
Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
Anapenda malumbano makali
Wanatumia nguvu
Jasiri
Wastahimilivu
Washindani
Wanauwezo ,
Wachunguzi wa mambo
Wasiri
Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
Wanajitegemea
Ni wenye maamuzi

#9 Nyota ya Mshale: Novemba 22 – Desemba 21
Ni alama ya moto na ni mwenye mapenzi mazito na vitu
Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
Ni mwenye kupenda uhuru
Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
Rafiki
Mwenye ari
Hawana utulivu
Waaminifu na wakweli
Wanapenda safari

#10 Nyota ya Mbuzi: Desemba 22 – Januari 19
Ni alama ya udongo na mwenye kuhitaji nyumba yenye amani ili kuhisi ukamilifu.
Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
Mgumu kubadilika
Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
Mfanyabiashara
Mwajibikaji

#11 Nyota ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18
Ni alama ya hewa:
Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
Wakipekee
Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
Mwenye huruma
Muona mbali
Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
Ana utu na mwenye kudai haki
Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
Anapenda sanaa na maisha ya anasa.

#12 Nyota ya Samaki: Februari 19 – Machi 20
Ni alama ya maji na ni mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo.
Ni mkweli na mwenye hisia nzito
Hana ubinafsi
Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
Mpenda amani
Ana huruma
Anajitoa
Wana ndoto
Wabunifu
Wana aibu
 
[Nyota ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18 Ni alama ya hewa:
Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria. Wakipekee Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake Mwenye huruma, Muona mbali, Mwenye ufahamu wa hali ya juu ni mbunifu, Anafanya marafiki wa aina mbalimbali Ana utu na mwenye kudai haki, Anapendwa na watu na anatengeneza urafiki kwa haraka... Anapenda sanaa na maisha ya anasa.]

KAMA KWELI VILE...... MNAJIMU UPO VIZURI
 
Aisee! Kumbe ndio nilivyo... Hiyo ya kukosa uvumilivu nimeshashindwa kuicontrol!
#1 Nyota ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19
Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
Kiongozi
Muongeaji
Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
Mwaminifu kwa marafiki na familia
Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi
 
Acheni ulozi

Yaan matapeli na watapeliwa wamehamia JF siku hizi

Muamini Muumba wako, acheni ramli

Mwishowe mtaabudu vitu vya angani

Hii elimu ya nyota chanzo chake ni MATAIFA YA KIPAGANI hasa wababeli,
 
VP KUHUSU NYOTA YA PUNDA MBONA WASEMA NYOTA YA PUNDA NI YA KWANZA AFU HAPO SIJA IONA KABISA NAOMBA UNIFAFANULIE
 
Back
Top Bottom