Nguvu ya mwanamke

Nguvu ya mwanamke

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
858
Kama Samson angeishi Dunia ya Sasa kwa ajili ya Delila angejinyoa nywele mwenyewe hakya nani....
=============================================
nimekuwa nikisoma mara kadhaa habari ya samson na delila....aisee "mkate hata uwe mgumu vipi kiboko yake chai". usione baba jeskeri anaogopwa sana na watu na wakati mwingine anataka kuonesha ukakamavu na kujenga hofu lakini ukimkuta kwenye yale maeneo mengine huwezi amini anavyokuwa.unaweza mkuta akiwa kama kifaranga cha kuku aliyenyeshewa na mvua. (tahadhali: jina la baba jeskeri ni jina la kubuni tu wala halihusiani na mtu yeyote aliye hai, mahututi au aliyekwisha fariki. ashakum si matusi)

hii dunia ya leo ukikaa ukatizama,ukasikiliza ukajisomea utagundua kabisa shetani yupo na Mungu yupo. hawa wadada wanavyowafanya wanaume .... we acha tu. unakuta baba mmoja kwake wanashindia ugali na maharage daily lakini kwa kumtoa out mchepuko na mashoga zake huo mchepuko acha kabisa. mara mlimani city,mara samaki samaki, mara huko mikocheni,mara mbezi. nyie akina dada mkumbuke kuna siku ya mwisho. shauri yenu.

nikawaza kwa ulimwengu huu wa sasa delila asingekuwa na kazi sana ya kumshawishi samson kuhusu nguvu zake. yaaani angemwambia tu hebu nieleze asili ya nguvu zako.samson angejifanya kidume then kuanzia hapo delila angekuwa akipigiwa simu na samsoni hapokei. akitumiwa meseji hajibu. status zake face book na whatsapp ingekuwa ni za madongo kwa samson kila akiamka anapost face book neno " mapenzi gani kama huwezi mwambia siri mwenzio" kesho akiamka " baba ukiona cha nini wenzako wanasema tutakipata lini" samson angemfuata delila mwenyewe na kumwambia nguvu zangu mimi ni kutokana na kutonyoa nywele na kama huamini ngoja nijinyoe uone.

hapo angechukua mkasi na kujipiga upara kichwa kizima halafu angelala kumwambia delila haya sasa kama huamini waite ndugu zako waje wanikamate uone kama nitakuwa na nguvu. nyie acheni tu wanawake wana nguvu kubwa sana. na wala silaha kali na ya maangamizi makubwa sana. na wala hawahitaji kunyanyua vyuma,kujifunza karate,kung fu au tai kwondo. wali‎
 
Eti baba jeskeri,tz bna full vituko
Umewaza nn sijui jamaa daaah
 
Hata iweje siwezi nikashindia ugali maharage then baadae nikamuhonge mwanamke hata awe mzuri kiasi gani!! WANAWAKE wana ushawishi ndio lakini sio wa kunifanya nishinde njaa kwa ajili yake
Unapingana na ukwel mkuu
 
Hata iweje siwezi nikashindia ugali maharage then baadae nikamuhonge mwanamke hata awe mzuri kiasi gani!! WANAWAKE wana ushawishi ndio lakini sio wa kunifanya nishinde njaa kwa ajili yake
mm hua nashindwa kwan
Hua wanashikiwa bastola
Maana mtu anaacha buku 5
Nyumban af akitoka anaenda


Kuspend 100000 kwa mtu ambae
Hana umuhimu wote
Huku family yako imeshindia
Ugali tembele

Ifke tu mahali wanaume tujitambue
Aiseee!! Kama hua hatuwekew
Limbwata
 
Makosa c ya mwanamke
Makosa n yetu kwann
Tutafute mchepuko wa garama

Tafta wa size yako
 
tatizo ni wanaume kutojitambua, kuwa kauzu kwa hawa viumbe weka msimamo na hasa ukizingatia una mke au mchumba wako
 
Unapingana na ukwel mkuu
Sio kupingana, ndio ukweli wenyewe huo....kushinda njaa nitashinda njaa kwa ajili ya Mama yangu na Familia yangu pekee(ili wao wale) sio kwa hao wanawake viruka njia mkuu.... Naanzaje kushindia ugali maharage kisa demu wa kudandia tu??
 
mm hua nashindwa kwan
Hua wanashikiwa bastola
Maana mtu anaacha buku 5
Nyumban af akitoka anaenda


Kuspend 100000 kwa mtu ambae
Hana umuhimu wote
Huku family yako imeshindia
Ugali tembele

Ifke tu mahali wanaume tujitambue
Aiseee!! Kama hua hatuwekew
Limbwata
Yaani ndio maana Lawama tunaletewa sisi wanaume hatuhudumii familia vizuri
 
Makosa c ya mwanamke
Makosa n yetu kwann
Tutafute mchepuko wa garama

Tafta wa size yako
Ni kweli kabisa ndugu yangu na ni ulimbukeni mi nilishajitambua kuhusu haya mambo,wala hayanipotezei muda kama ni mchepuko natafuta muuza karanga au ubuyu ambae nikimpa buku 3 au nne anashukuru anapiga hadi magoti!!! Lakini hawa wanawake wa mitoko mi nilishasema NO
 
Huo ni ulimbukeni wa mapenzi na kutojiheshimu kwanini uwe na mchepuko wakati umeoa au kuolewa nawasihi mutafute mke mwema kama Me too
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom