Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Bobi Wine ameachiwa huru leo na inadaiwa ni kutokana na shinikizo toka Ubalozi wa Marekani nchini Uganda,

Hana kesi ya kujibu.

Chanzo: City Radio Uganda

=======

Taarifa za hivi punde kutoka Uganda ni kwamba mahakama ya jeshi imemuondolea mashtaka mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi.

Inaarifiwa kwamba mahakama hiyo ya jeshi inataka badala yake inataka kumkabidhi mbunge huyo kwa mahakama ya kiraia ajibu mashtaka ya uhaini pamojana wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo alitarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru.
=========

UPDATE
Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom